HEADER AD

HEADER AD

MADIWANI WALALAMIKA ZAHANATI KUTOKUWA NA MTAALAM WA MAABARA


Na Daniel Limbe, Chato

LICHA ya Serikali kuendelea kuboresha huduma za afya nchini kwa kujenga Hospita,Vituo vya afya na Zahanati bado tatizo la watumishi limetajwa kuwa kikwazo wilayani Chato mkoani Geita.

Wakizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Chato cha kuwasilisha taarifa za Kata Februari 16, 2023, Diwani wa Kata ya Ichwankima Denis Joseph, ameeleza kuwa Zahanati ya kijiji cha Ichwankima haina mtaalamu wa maabara hata mmoja jambo linalo wawia vugumu wauguzi wengine kutimiza majukumu yao.

Mbali na hilo, amesema baadhi ya wagonjwa wanalazimika kutumia gharama kubwa pamoja na kutembea umbali mrefu kuzifikia huduma za vipimo kwenye kutuo cha afya Kachwamba na wengine kwenda hospitali ya wilaya ya Chato.

                  Madiwani wakia kikaoni

"Mwenyekiti tatizo hili nililiwasilisha kwenye kikao cha Baraza lililopita na baraza lako likatoa maamuzi ya kuletewa mtaalamu huyo ndani siku saba, ajabu mpaka leo sijaletewa mtumishi huyo" amesema Joseph.

Kutokana na hali hiyo, baraza hilo limempa siku moja Mkurugenzi  Mtendaji wa halmashauri hiyo kuhakikisha Zahanati hiyo inapelekewa mtaalamu wa maabara ili kunusuru maisha ya wagonjwa kwenye kijiji hicho.

"Mkurugenzi tulikuagiza ndani ya siku saba uwe umepeleka mtaalamu pale Ichwankima, nashangaa kusikia hukutekeleza agizo hilo, sasa tunakuagiza tena kesho hakikisha tayali mtumishi huyo awe amefika kwenye zahanati hiyo.

"Diwani nakuomba tuwasiliane kufikia kesho iwapo mtaalamu huyo atakuwa hajaletwa" amesema Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Photunatus Jangole.

Hata hivyo, Kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Gerald Mgoba, ameahidi kulishughulikia suala hilo haraka ili kuondoa adha iliyopo kwa wananchi hao.

                        

No comments