UKARABATI BARABARA YA LUSAHUNGA- RUSUMO KUFUNGUA FURSA YA KIUCHUMI.
Na Mwandishi Wetu, Kagera
MKUU wa mkoa wa Kagera Albert Chalamila amesema kuwa barabara ya Lusahunga-Rusumo yenye urefu wa km 92 ikikarabatiwa kwa kiwango cha lami itafungua fursa za kiuchumi kati ya nchi za Rwanda, Burundi na Tanzania.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa habari juu ya afla ya utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo utakaofanyika februari 18, 2023 Benaco ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Pro.Makame mbalawa.
Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa ukarabati wa barabara hiyo utasaidia kuondoa vikwazo vilivyopo vitokanavyo na uchakavu wa barabara na hivyo kufungua fursa za biashara kwa kurahisisha huduma ya usafirishaji na kwamba itainua uchumi wa Kagera na Tanzania kwa ujumla.
" Kwa kutambua umuhimu wa barabara hii Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameona ni mwafaka kufungua uchumi wa mkoa wa Kagera na Tanzania kwa ujumla.
"Nawaalika wananchi wetu, vyama vya siasa Taasisi mbalimbali zikiwemo za dini, Mashirika ya Umma na yasiyo ya umma, Wataalam ili kushuhudia kasi kubwa anayoifanya Rais Samia katika kuwaletea wanachi maendeleo" amesema Albert.
Ameongeza kuwa Serikali imeidhinisha kiasi cha dolla Milioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa maegesho ya magari Benaco, jengo la utawala la halmashauri ya Ngara, na soko la kisasa Rusumo wilaya ya Ngara zinazotarajiwa kupokelewa.
Post a Comment