HEADER AD

HEADER AD

MARIE STOPES YAFIKA MAJUMBANI KUTOA HUDUMA YA AFYA KWA WAGONJWA


Na Jovina Massano, Musoma.

KATIKA kuhakikisha wagonjwa wasioweza kutembea wakiwemo wazee wanapata huduma ya matibabu, Kituo kinachotoa huduma ya afya Marie Stopes Polyclinic kilichopo Manispaa ya Musoma mkoani Mara kimekuwa kikifika majumbani kutoa huduma ya uuguzi kwa wagonjwa. 

Akizungumza na Mwandishi wa DIMA Online, Meneja Msimamizi wa Marie Stopes Polyclini, Frank Lacksung'uda amesema lengo la kutoa huduma hiyo ni kuwawezesha wagonjwa wasiojiweza kutembea kupata matibabu kwa wakati badala ya kulazimika kuifuata huduma ya afya hospitali.

"Kituo chetu kinawafikia hadi wagonjwa walioko majumbani wasioweza kutembea au wazee wenye umri mkubwa, tukipata taarifa kuwa kuna mgonjwa anahitaji matibabu tunamfuata na kumpatia huduma ya uuguzi nyumbani kwake, pia tunatoa huduma za safari ya mama kuelekea kujifungua.

Amesema Kituo cha Marie Stopes Polyclinic kina madaktari bingwa, hutoa huduma za kibingwa kwa magonjwa ya kina mama na watoto, magonjwa ya ndani kama vile shinikizo la damu(Blood Pressure), Sukari, Figo na mengineyo ambapo kwa sasa kimeongeza huduma ya daktari bingwa wa mifupa.

"Pamoja na hayo tunatoa huduma za afya kwa ujumla ambayo utamuona daktari utafanyiwa vipimo. Tunapokea bima zote binafsi na za Serikali sambamba na hilo tupo muda wote saa 24.

"Tunawataarifu wananchi msipate changamoto yeyote nyakati za usiku kwa sasa Marie Stopes iko wazi kwa ajili ya kuhudumia wananchi", amesema Frank.

Frank ameongeza kusema, vipimo vingine vinavyotolewa ni pamoja na kipimo cha moyo cha ECG na ECHO, kipimo cha homoni zote kwa ujumla, kipimo cha Ini na Figo, huduma ya mifupa ambayo hufanyika kuanzia saa kumi jioni na kwamba gharama za huduma ni nafuu kulingana na tatizo la mgonjwa.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi wameupongeza uongozi wa Marie Stopes Polyclinic kwa utoaji huduma saa 24 na kwenda kutoa huduma majumbani kwa wagonjwa wasioweza kutembea kufuata huduma Hospitali.

Mkazi wa Iringo B Manispaa ya Musoma Asnati Juma ameupongeza na kuushukuru uongozi wa kituo cha madaktari bingwa (Mariastopes Polyclinic) kwa kutoa huduma saa 24 ambayo imesaidia kupata matibabu hata wanapofika nyakati za usiku.

                 Asnati Juma

"Nimefurahi sana kwasababu huduma za uzazi wa mpango zinapatikana, hata za mama na mtoto lakini pia hata ukiwa na maradhi mengine na gharama zao ni nafuu na wanapokea bima za afya wako vizuri", amesema, Asnati.

Naye Lameck Kadoshi miongoni mwa wanaopata huduma ya afya katika kituo hicho amewapongeza wafanyakazi wa Marie Stopes kwa kuhudumia vizuri  wagonjwa.

                  Lameck Kadoshi

"Ukifika unapokelewa vizuri  na wahudumu, wapo makini wanaelewa wajibu wao, lugha zao ni nzuri wanakusikiliza, hii ni mara yangu ya pili nafika hapa kwa ajili ya kupata matibabu nafurahia sana huduma zao ",amesema Lameck.





            

No comments