TAKUKURU RAFIKI YATUA BUNDA
Na Mwandishi Wetu, Bunda.
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilayani ya Bunda mkoani Mara imetambulisha programu TAKUKURU- rafiki kwa Madiwani na Wakuu wa Idara katika Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Bunda Mohamed Paul ametambulisha programu hiyo Februari, 7, 2023, lengo likiwa ni kufungua milango ya kushirikiana kwa pamoja na wananchi katika kuzuia rushwa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Michael Kweka akiongea kwa niaba ya Madiwani wa halmashauri hiyo, amesema wanaunga mkono programu ya TAKUKURU - Rafiki kwa kuwa inaenda kuondoa changamoto ya kero kwa wananchi pamoja na kusaidia miradi ya maendeleo.
Post a Comment