HEADER AD

HEADER AD

WAKAMATWA KWA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI

Na Alodia Babara, Bukoba

JESHI la Polisi mkoani Kagera linawashikilia watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majangili kwa tuhuma za wizi wa nyara za Serikali katika Hifadhi ya ya Taifa Ibanda - Kyerwa pamoja na silaha mbili aina ya Gobore na risasi tatu za kienyeji aina ya goroli.

Kamishna Msaidizi wa uhifadhi, Hifadhi ya Taifa Ibanda –Kyerwa Fredirick Mofuli akiongea na waandishi wa habari  Februari 19, 2023 amesema kuwa tukio la kuwakamata watu hao na nyara za Serikali lilitokea Februari 13,2023 majira ya saa tatu  usiku katika vijiji vya Muungano na Lusahunga wilaya ya Biharamlo mkoani hapa.


Amesema ukamataji ulipangwa na kufanikiwa baada ya kupata taarifa za kiinterejensia za uwepo wa mtandao wa watu wanaojihusisha na ujangili wa wanyamapori pamoja na biashara ya nyara za Serikali.

Nyara hizo ni meno mawili ya tembo, ngozi ya fisi, kichwa cha fisi, vipande vitatu vya ngozi ya nyati, mkia wa nyati, ngozi ya swala aina ya pala na  siraha  mbili aina ya Gobore na risasi tatu za kienyeji aina ya goroli.

                Nyara za Serikali

“ Meno yote mawili ya tembo yana uzito wa kilogram 9.15 na Kati ya meno ya hayo yaliyokamatwa jino moja lenye alama ya A lina uzito wa kilogram 4.75 wakati jino la pili lenye alama A1 likiwa na uzito wa kilogram 4.40” Amesema Fredrick.

Aidha Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kagera Wiliam Mwampaghale amesema jeshi hilo linawashikiria watu wanne kwa tuhuma za ujangili ambao ni Raphael Lugaira (44), Fikiri Rugaira ( 43), Majaliwa Charles (42) na Warwa Rupilya  (45) wote wakazi wa wilaya ya Biharamlo mkoani Kagera na kuwa watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.

Kamishna msaidizi wa uhifadhi, hifadhi ya Taifa Rumanyika –Karagwe Charles Ngendo amesema wanatoa rai kwa watanzania wote kutojihusisha na vitendo vya ujangili dhidi ya maliasili kwani jeshi hilo ni imara na kwamba yeyote atakayejihusisha na vitendo vya ujangili atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.



No comments