HEADER AD

HEADER AD

WANANCHI MUSOMA WATAKIWA KULINDA MIUNDOMBINU YA BARABARA

Na Jovina Massano, Musoma


WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Halmashauri ya Manispaa ya Musoma Mjini Mkoani Mara amewaomba wananchi na wadau wote kushiriki kikamilifu katika kulinda miundombinu ya barabara.

Hayo yameelezwa na Kaimu Meneja wa TARURA, Mhandisi Mohamed Etanga February 22/2023 wakati akisoma rasimu ya bajeti ya TARURA kwa mwaka wa fedha 2023/2024, kwa niaba ya  Meneja wa TARURA Wilaya hiyo, Mhandisi Joseph Mkwizu katika kikao Cha baraza la Madiwani Halmashauri hiyo.

Amesema moja ya changamoto iliyopo ni ufanyaji wa shughuli za kibinadamu hasa biashara zisizozingatia taratibu na kwamba kwa mwaka huu wa fedha 2023/2024, TARURA imepanga kutumia kiasi cha Tshs Billion 4.8.

     Mhandisi Mohamed Etanga TARURA

Fedha hizo ni kwa ajili ya matengenezo ya barabara,ujenzi wa madaraja,makalvati na mitaro ya kupitisha maji ya mvua katika Manispaa ya Halmshauri ya Musoma.

"Kutokana na ukiukwaji wa sheria ya Barabara  TARURA  imedhamilia kuchukua hatua kwa kuanza kutoa elimu ili kufanikisha kulinda miundombinu ya barabara". amesema Mohamed.

Ameongeza kuwa takwimu ya Manispaa ya Musoma ina mtandao wa barabara yenye urefu wa km 233.21 zikiwemo za lami km 23.78, changalawe 108.04 na za udongo km 101.39  hivyo  basi katika mpango huu wa rasimu ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/2024 km 41 za changalawe zinatarajiwa kufikiwa.

           Madiwani

Sanjari na hayo baraza la madiwani Manispaa ya Musoma wameipongeza TARURA kwa usimamizi bora wa ujenzi wa barabara.

Mwenyekiti wa Baraza Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo William Gumbo amesema"Ninyi ni mashahidi TARURA wamekuwa wasikivu  pindi kunapokuwa na dharura ni wepesi kuitikia na kutekeleza tunawapongeza sana.

    Mwenyekiti wa Baraza Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo William Gumbo

" Lakini pia nawaomba taarifa zao za miradi maeneo husika zifike mapema kwa viongozi wa eneo husika ili kusiwe na maswali mengi wakati wa utekelezaji".

Nae Diwani wa Kata ya Nyakato Joseph Kisunda amesema Kata yake imepewa km 2 na kwamba bajeti hiyo itasaidia wananchi hususani barabara, kalvati na mitaro hususani maeneo ya SDA,Tanesco kuelekea gengeni hadi msikitini.

Philipo Nyambaya mkazi wa Karume Manispaa ya Musoma amewaomba TARURA kutoa elimu ya kina ya utunzaji wa mazingira na miundombinu ya barabara kwani kodi zinazotoka kwa wananchi ndio zinazofanya maendeleo.

               Watendaji 
         

No comments