HEADER AD

HEADER AD

DC CHATO: WAKULIMA ACHENI KILIMO CHA KUKARIRI.


Na Daniel Limbe,Chato

SERIKALI wilayani Chato mkoani Geita,imewataka wakulima kubadili fikra za kilimo cha mazoea badala yake wajikite kwenye kilimo kitachowapatia tija kwa haraka.

Mkuu wa wilaya hiyo, Deusdedith Katwale, ametoa rai hiyo wakati akizungumza na wanachama wa Chama kikuu cha ushirika wilaya ya Chato (CCU) kwenye mkutano mkuu wa kawaida wenye lengo la kupitisha makisio na ukomo wa madeni kwa msimu wa kilimo 2023/24.

     Mkuu wa wilaya ya Chato,Deusdedith Katwale,akitoa nasaha zake kwa wanachama wa chama kikuu cha ushirika wilaya ya Chato(CCU)

"Haiwezekani wakulima wetu kuendelea na kilimo cha kukariri lazima tukubali kubadilika kifikra tunaweza kulima pamba sawa lakini pia mazao mengine kama tumbaku, mpunga na alzeti tunahitaji wakulima wetu wanufaike na kilimo chao" amesema

"Hakuna sababu ya wakulima wetu kuendelea kuwa maskini tatizo lipo kwetu viongozi hatujawaelimisha wananchi kuzitumia fursa za kilimo kujikwamua na wimbi la umaskini nikingali nipo Chato sitokubali hali hii kuendelea lazima tuwajibike kwa wananchi wetu".

Kauli hiyo,imepokelewa kwa shangwe kubwa baada ya wajumbe wa mkutano huo kutoka Amcos 54 ambazo ni wanachama cha CCU, kumshangilia mkuu huyo wa wilaya, ikiwa ni ishara ya hotuba yake kugusa nyoyo zao.

Mwenyekiti wa CCU, Greon Chandika na Kaimu meneja wa Chama hicho,Beno Msigwa,wamesema wanatarajia kuchukua mkopo wa zaidi ya 1.4 bilioni kwaajili ya kusimika mitambo mipya ya kukamua mafuta ya kula yatokanayo na pamba.

       Mwenyekiti wa Chama kikuu cha ushirika wilaya ya Chato(CCU) Greon Chandika,akizungumza na waandishi wa habari

"Ni matarajio yetu kwa msimu mpya wa 2023/24 tunakwenda kufanya mageuzi makubwa ya kibiashara tunatarajia kusimika mitambo mipya ya kukamua mafuta ya pamba ikiwa ni jitihada za kuisaidia serikali kukabiliana na changamoto ya upungufu wa mafuta ya kula nchini" amesema Chandika.

Mbali na mafuta,pia tutaendelea na kilimo cha mazao mengine ya kibiashara ambapo zaidi ya Amcos zetu 19 zimeonyesha mpango mzuri wa kilimo cha tumbaku inayokaushwa kwa hewa badala ya ile ya kukausha kwa moshi.

     Kaimu Meneja mkuu wa Chama kikuu cha ushirika wilaya ya Chato(CCU) Beno Msigwa,akizungumza na waandishi wa habari.

"Tumbaku ya kukausha kwa hewa ni rafiki kwa mazingira baadhi ya wakulima wetu wameanza kuichangamkia fursa ya kilimo hicho, hata hivyo tunao mpango mkakati wa kuyafufua mashamba yetu yaliyopo Nyakato Buzirayombo kwaajili ya kilimo cha mpunga" amesema Msigwa.

        Mwonekano wa kiwanda cha CCU kinachofanya kazi ya kuchambua pamba,kufunga robota na kukamua mafuta ya kula.

       Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa CCU wakiendelea kusikiliza maelekezo mbalimbali toka kwa viongozi

No comments