KANISA KATOLIKI LAMJIBU KIAINA MZEE MAKAMBA
Na Daniel Limbe,Chato
KATIKA kile kinachoonekana ni kujibu propaganda za aliyewahi kuwa Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (CCM) Yusuph Makamba, Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge Ngara, limesema hata watu wema hufa.
Kauli hiyo imetolewa na Askofu wa Kanisa hilo,Jimbo la Rulenge Ngara,Severine Niwemugizi wakati akiongoza ibada ya kumwombea toba aliyekuwa rais wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.
Ni katika Ibada iliyoambatana na kumbukizi ya miaka miwili ya kifo cha Hayati Dk. Magufuli iliyofanyika kwenye Parokia ya Mlimani Rubambangwe Chato na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali,Chama cha CCM,familia pamoja na wananchi mbalimbali.
Mwonekano wa msafara magariKiongozi huyo amenukuu maandiko kutoka kitabu kitakatifu cha Biblia, yaliyoandikwa na mfalme Suleiman ambapo amesema siyo wabaya tu wanaokufa bali hata wema hufa,ndiyo maana hata Yesu kristo alikufa akiwa na umri wa miaka 33 pamoja na kwamba alikuwa mtakatifu.
Askofu Severine Niwemugizi,akiweka baraka kwenye kaburi la Hayati Dk. Magufuli"Yesu kristo alikufa akiwa na miaka 33 je, alikuwa mbaya watoto wanazaliwa na kufa, vijana kingali wadogo wanakufa je nao huwa ni wabaya" alihoji Askofu Niwemuzigi.
Kauli hiyo ya askofu ametafsiliwa ni kujibu propaganda za aliyewahi kuwa Katibu mkuu wa CCM Taifa,Yusuph Makamba, ambaye alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari wakati wa kikao cha kwanza cha mkutano mkuu CCM uliolenga kumthibisha mwenyekiti wa Chama hicho taifa, baada ya kifo cha Hayati Magufuli ambapo alisema watu wazuri hawafi.
Licha ya kauli hiyo kukosolewa vikali kwenye mitandao ya kijamii, siku moja baadaye rais Samia Suluhu aliwaomba radhi watanzania wakati akihitimisha mkutano mkuu wa 10 wa Chama hicho na kudai kwamba Mzee Makamba aliteleza ulimi kwa kuwa hakuwa na nia mbaya.
Ibada ya kumwombea Hayati Magufuli ikiendelea kwenye kanisa la Katoliki Parokia ya MlimaniAkitoa salaam kwa niaba ya familia, mke wa Hayati Magufuli, Janeth Magufuli, amelipongeza kanisa Katoliki kwa kuenjdelea kuungana na familia hiyo,kumwombea mpendwa wao ambaye ametimiza miaka miwili tangu umauti ulipomkuta.
Akitoa salaam za serikali kwa niaba ya rais Samia Suluhu Hassan,Waziri wa Ulinzi, Inocent Bashungwa,amemuelezea Hayati Dk. Magufuli kuwa ni kiongozi atakaye kumbukwa na vizazi vingi kutokana na maendeleo makubwa aliyotekeleza enzi za uhai wake.
Waziri wa Ulinzi,Inocent Bashungwa akinena Jambo na aliyekuwa Katibu mkuu wa fedha kipindi cha serikali ya awamu ya tano,Doto James."Hayati Dk. Magufuli ataendelea kukumbukwa na serikali na jamii kwa alama kubwa alizoziacha kwa nchi yetu, rais Samia amenituma kufikisha salaamu hizi kwa familia na kwamba anaendelea kuwakumbuka katika siku hii muhimu"amesema Bashungwa.
Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati John Pombe MagufuliAliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli wakati wa uhai wake.
Post a Comment