MWENYEKITI ALIYESIMAMISHWA UONGOZI MAGUNGA AFUNGUKA
Na Dinna Maningo, Butiama
MWENYEKITI wa Kijiji cha Magunga Kata ya Mirwa Wilaya ya Butiama mkoani Mara, Magige Mahera Msyomi aliyesimamishwa uenyekiti wa kijiji na Chama cha Mapinduzi (CCM) anasema kuwa kusimamishwa kwake kunatokana na chuki za baadhi ya viongozi wa chama.
Novemba, 10, 2022 Chama cha Mapinduzi ngazi ya Wilaya kilimsimamisha uongozi yeye pamoja na wajumbe watatu wa Serikali ya Kijiji ambao ni Joseph .M. Wambura, William Mriri Ghati na Juma Jumbe Wilson kwa tuhuma saba zikiwamo za matumizi mabaya ya madaraka.
Kusimamishwa kwa viongozi hao kumeibua sintofahamu kwa wananchi kwakuwa hawajawahi kutangaziwa kwenye mkutano mkuu sababu za Chama kuwasimamisha uongozi Mwenyekiti wa Kijiji na Wajumbe.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho anasema yeye amekuwa ni mfuatiliaji wa miradi ya maendeleo na anaposimamia miradi baadhi ya viongozi wa CCM wenye maslahi binafsi ya kifedha umwandama na kumtengenezea migogoro ili aonekane mtu mbaya.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Magunga aliyesimamishwa uenyekiti na Chama cha Mapinduzi, Magige Mahera Msyomi
Anasema amesimamishwa uongozi bila taratibu sahihi kufuatwa kwani si yeye tu kusimamishwa uongozi wapo na Wenyeviti wengine wawili kabla yake walisimamishwa uongozi na nafasi zao kukaimishwa wajumbe wengine walioshikilia madaraka na kuachia ilipofika wakati wa uchaguzi.
Anasema Kijiji cha Magunga kina vyanzo vya mapato kama vile shamba la Kijiji, soko, vibanda, machinjio mnara wa Vodacom, ushuru wa magari yanayotoka na kuingia kijiji cha Magunga, mradi wa maji wa mtandao wa mabomba,Kisima cha Kupampu, mgodi wa Wachimbaji wadogo wa madini na mnada.
Vibanda vya wajasiriamali kila mwaka Kodi ya pango la ardhi ni sh. 30,000 inayokusanya na serikali ya Kijiji cha Magunga
Anasema katika vyanzo hivyo chanzo cha vibanda na maduka yaliyopo sokoni, kisima cha maji cha asili ndiyo vinajulikana mapato yake lakini miradi mingine haijulikani kiasi kianchokusanywa na matumizi yake, anapohoji uchukiwa na kuitwa mpinzani.
Anasema kuna kamati zimeundwa kusimamia utendaji kazi lakini baadhi ya wajumbe hawashirikishwi kujua lolote kuhusu miradi kwakuwa Mtendaji wa Kijiji hicho Lucus Kagina hana uwazi katika makusanyo ya fedha na hasomi mapato na matumizi ya kijiji hicho.
Anaeleza kwamba Mtendaji huyo wa Kijiji amekuwa si muwazi katika makusanyo ya fedha hususani zinazotolewa kutekeleza miradi ya maendeleo.
Anasema Mtendaji na viongozi wa CCM Kata pamoja na Diwani wa Kata hiyo Willy Brouwn wamekuwa wakishirikiana kuhujumu miradi ya maendeleo kupitia nafasi zao za uongozi hali inayopelekea miradi kujengwa chini ya kiwango kwakuwa fedha uingia kwenye mifuko ya viongozi hao.
"Kuna shamba la Kijiji la ekali 65 ambalo wananchi wanakodi kulima mazao kila ekali ni sh.30,000 kwa kila msimu wa kilimo, kuna kisima cha asili cha kiomari ambacho mzabuni analipa Kijiji Tsh. 55,000 kila baada ya miezi mitatu, kuna Kodi ya pango la ardhi kwa wafanyabiashara wenye vibanda sokoni wanalipa Tsh. 30,000 kwa kila mwaka.
"Hivyo vyanzo ndiyo vinajulikana makusanyo yake lakini vyazo vingine makusanyo hayajulikani hata vile vinavyokusanywa na halmashauri Kijiji hatujui wanakusanya sh. ngapi ili tujue gawio linalostahili kijiji kupatiwa"Anasema Magige.
Anavitaja vyanzo vya mapato ambavyo Kijiji hakifahamu makusanyo yake vikiwemo vinavyosimamiwa na halmashauri ya wilaya ya Butiama huku akiomba Serikali pale inapokusanya mapato ni vyema Serikali ya Kijiji ikajua kiasi kinachokusanywa kwa kuwa ni miradi iliyopo kijijini.
"Tuna mnada wa kila jumamosi Halmashauri inakusanya sh. 1000 kwa kila mfanyabiashara, ushuru wa mifugo, kuna maegesho ya magari ushuru sh 1000 kwa magari madogo na kila roli sh. 5,000, kuna mgodi wa Dhahabu Halmashauri ya wilaya inatoza kila kiroba sh. 1,000 pesa zinazokusanywa na halmashauri lakini hatujui kiasi kinachokusanywa na gawio kwa mwaka kutoka halmashauri katika kutekeleza miradi.
"Kuna Machinjio inayomilikiwa na Katibu wa CCM Kata kwa siku wanachinjwa ng'ombe wasiopungua 5, mbuzi na kondoo kwa siku ni kati ya 20-40, ng'ombe anapochinjwa mmiliki wa machinjio analipwa 12,000 kwa kila ng'ombe mmoja na kwa mbuzi na kondoo ni sh. 6,000.
"Pia kuna eneo la stendi tulitenga ili gari zikae huko lakini wakapinga, gari zinaendelea kujibana pembezoni mwa barabara wakati kuna eneo la stendi ambalo gari zinaweza kupaki kuliko yanavyojibana pale yalipo sasa" anasema Magige.
"Cha kushangaza hatujui mapato yanakokwenda, kuna sheli ya mafuta inayomilikiwa na Afisa Mifugo Kata ya Mirwa, inatakiwa kulipa tozo ya huduma sh 30,000 kwenye halmashauri ya kijiji lakini haijawahi kulipwa" anasema Magige.
Anazidi kuongeza " Kuna mnara wa Vodacom upo karibu na shule lakini Kijiji hakinufaiki hata kusaidia shule iliyo karibu na mnara yenye upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa, kama wenye vibanda wanalipa kodi kwanini mnara haulipi CSR!.
"Kuna wachenjuaji wa Dhahabu tangu walipokipatia Kijiji mabati 180 ikawa ndiyo baibai, hatujui wao wanalipa wapi mapato, Mgodi hatujui unalipa wapi fedha za CSR, kuna kisima kilichokuwa cha Hesawa ambacho ni cha jamii lakini fedha anakusanya mtu mmoja ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maji anaweka mfukoni mwake Kijiji hakinufaiki"anasema Mwenyekiti.
"Nilipoanza kufuatilia kuhusu vyanzo hivyo ndipo nikaingia kwenye matatizo kwasababu baadhi ya miradi inamilikiwa na viongozi hao wa Chama, yaani akitokea Mwenyekiti wa Kijiji anauelewa na kuhoji kuhusu fedha na miradi unatengenezewa mizengwe, na kwakuwa wana pesa wanafanya wanachokitaka, wamekeweza miradi lakini Kijiji hatujui mapato wanayotoa." anasema.
Ajibu tuhuma zilizosababisha asimamishwe kazi
Octoba, 31, 2022 Chama cha Mapinduzi CCM ngazi ya Kata kilimsimamisha uenyekiti wa Kijiji na kikaandika barua ya kero kwenda ofisi ya CCM Wilaya ya Butiama kikimtuhumu kuhusika na makosa saba yeye na wajumbe watatu.
Chama ngazi ya Kata kilieleza kuwa kikao kimekubali avuliwe dhamana ya Chama na kwamba kwa maelekezo ya Chama ofisi ya Kijiji imekabidhiwa Mtendaji wa Kijiji na Wenyeviti wa Vitongoji mpaka ushauri utakapotoka juu.
Baada ya kusimamishwa uongozi imeelezwa Chama hicho kilimpa majukumu mjumbe wa halmashauri ya Kijiji hicho, Daud Sarurya kukaimu uenyekiti wa kijiji bila wananchi kushirikishwa na kutambulishwa kupitia mkutano mkuu wa wananchi na ndiye ameshikilia ofisi na kusimamia shughuli zote za Kijiji.
Mwenyekiti anasema tuhuma zinazomkabili ni za kupika na za chuki
binafsi na kwamba awali Chama kilimsimamisha uenyekiti na nafasi yake kurejeshwa lakini wabaya wake wameendeleza njama kuhakikisha anaenguliwa uongozi na wamefanikiwa kumsimamisha uenyekiti.
" Wanasema mimi sisomi mapato na matumizi anayepaswa kusoma mapato ni Mtendaji wa Kijiji Lucus Kagina ambaye amekuwa hanipi ushirikiano yeye anafanya kazi na viongozi wa Chama siye wengine hana habari na sisi yeye ndiye anatakiwa asome mapato na matumizi yeye ndiyo mhasibu na mkusanya mapato, mimi ni kuitisha mkutano na kusimamia tu.
"Kutopewa ushirikiano na Mtendaji wa Kijiji ilipelekea mimi kuandika barua Septemba,02,2020 kwenda kwa Mkuu wa wilaya Butiama nikimlalamikia mtendaji kupeleka mihitasari ya vikao vya Halmashauri ya Kijiji bila sahihi yangu na kutoa fedha benki kabla ya vikao kujadili.
"Mtendaji wa Kijiji anaandika mihitasari ya halmashauri ya Kijiji na ya mkutano mkuu wa Kijiji na kwenda kufanyia kazi pasipo mimi kuweka saini yangu na anakwenda kuchukua fedha za miradi benki, kama fedha za Zahanati na choo cha mnada na kutumia fedha hizo pasipo kufuata taratibu stahiki" anasema Mwenyekiti huyo.
Zahanati Kijiji cha Magunga iliyojengwa kwa nguvu za wananchi hadi kukamilika boma na serikali ikatoa Milioni 50 kupauwa n kukamilisha na Milioni 16 za serikali ya Kijiji lakini bado haijakamilika
Anaongeza "Nililalamika kuwa ashirikishi wananchi au wajumbe wa halmashauri ya Kijiji hali ambayo imesababisha ujenzi kutoendana na gharama za fedha iliyotolewa benk.
"Nilieleza kwamba Mtendaji amekuwa akinizunguka na hatambui dhamana niliyopewa ndani ya Kijiji, kuna miradi ambayo imejengwa chini ya viwango licha ya fedha nyingi kutolewa, anatumia mahudhulio ya vikao na kwenda kujiandikia mihitasari na kufanya majukumu pasipo kusaini baada ya ajenda ya mwisho ya kufunga kikao.
Magige anasema kupitia barua hiyo aliomba mihitasari iliyotoka Kijiji cha Magunga iliyopo ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ikaguliwe na hatua zichukuliwe kwa muda mwafaka ili jina lake lisiwe linachafuliwa kwa ujenzi unaokuwa chini ya viwango.
" Niliandika barua hiyo na nakala nikatuma kwa Katibu Tawala mkoa wa Mara kwa ujulisho na ufuatiliaji,Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Butiama alione kwa uzito wa juu kwa mtumishi huyo,Mtendaji Lucus Kagina, Mtendaji Kata ya Mirwa na Mkutano mkuu wa Kijiji kwa Taarifa.
" Wanasema nimekwamisha ujenzi wa choo cha mnadani, tulipewa maeno tukaweka vibanda na tunalipia, ujenzi umekuja ukakuta kibanda changu, wakasema nirudi nyuma kidogo ili choo kijengwe waongenze matundu mengine.
"Nilitii sikujali kuwa mradi umenikuta nikasogeza hatua walizotaka lakini hadi leo ujenzi hujafanyika, juzi nimeona baada ya mwandishi kuandika ndiyo wameenda mafundi kijenga kwasababu walijua wakaguzi wakati wowote wanaenda kukaga" anasema Magige.
Anaongeza " Kuna choo cha sokoni niliingia madarakani nikakuta limechimbwa tu shimo tukajenga choo kwa zaidi ya Milioni mbili lakini tukashindwa kuendeleza baada ya mmiliki wa sheli ya mafuta ambaye ni Afisa Mifugo Kata ya Mirwa Washington Benasus kukatalia kipande cha eneo akidai ni eneo lake ujenzi umekataa kuendelea.
Anaongeza " Kijiji kililalamika halmashauri tukasikilizwa Mhandisi ujenzi Bakari S.Mwijarubi mwezi Februari, 14, 2022 alitoa kibali kuendelea na ujenzi lakini Washington amekataa kuachia eneo ili ujenzi iendelee.
" Choo kimeshindwa kuendelezwa kwasababu mmiliki wa sheli aliyepewa eneo na kijiji alijiongezea eneo, wafanyabiashara wamekosa mahali pakujisaidia na ushuru wanalipa anakatalia eneo ambalo ni la kijiji"anasema Mwenyekiti huyo.
Kuhusu kutoa taarifa za uongo kwenye vyombo vya habari amesema " Kila mtu ana haki ya kufanya kazi na vyombo vya habari hata serikali yetu huwa naona viongozi wakiambatana na Waandishi wa habari kwenda kuandika habari kwenye ziara zao.
Niliita Mwandishi wa Habari kuandika habari kwenye Kijiji zikiwemo za changamoto na alipoziripoti kwenye vyombo vya habari Serikali ilituletea zaidi ya Milioni 47 vikajengwa vyumba vya madarasa shule ya msingi Kamimange, Milioni 25 ikaletwa ikajenga nyumba ya mwalimu mkuu shule Magunga.
"Serikali ikaleta Milioni 50 ujenzi wa Zahanati. Kama ulikuwa uongo mbona hatua zilichukuliwa? na unaficha ili isaidie nini, yaliyoandikwa yalikuwa ya kweli, sema wao walitaka yawe siri kwasababu ya madudu yao" anasema Magige.
Kuhusu kuchukua matofari 500 ya Umoja wa Vijana (UVCCM) na mawe anasema" Kuna uwanja wa Serikali ya Kijiji ambao vijana waliomba wautumie kucheza mpira, wakawa wakitaka kucheza wanabadilisha nguo hadharani, nikatafuta mdau mimi mwenyewe.
"Nikamuomba anisaidie matofari ili wajenge chumba cha kujistili, tukawajengea lakini CCM Kata wakaniamuru niondoe kwamba uwanja ni wa Chama wakasema nipeleke nitakapojua nikaondoa na kupeleka kwangu, hayakuwa matofali ya Chama" anasema.
Akizungumzia tuhuma za kumtoza mwananchi fedha Tsh. 367,00 bila stakabadhi ya Kijiji na kufanyia shughuli zake amesema.
"Kuna mwananchi alijenga nyumba kwenye eneo la mtandao wa maji watu wakakosa maji tulipofuatilia tukagundua alikuwa amekata bomba, akajihukumu mwenyewe kulipa faini ya kiasi hicho cha fedha.
"Kwakuwa hakukuwa na vitabu vya stakabadhi ya malipo tukamsainisha kwenye karatasi akasaini na mimi nikasaini tukiwa na mjumbe aliyekuwa Katibu wa Kamati ya mipango na fedha tukazipeleka kwenye ujenzi wa choo cha sokoni.
Anaongeza "Wakati huo Kijiji kilikuwa hakina Mtendaji baada ya aliyekuwepo kukimbia akituhumiwa kula fedha za vitambulisho vya wajasiriamali, baadae Mkurugenzi aliyekuwepo Diana Sonno alituonya kutumia fedha kabla haijaenda benk akatuelekeza kuwa tukikusanya fedha iende kwanza benk kisha ndiyo ikafanye maendeleo swala hilo likaisha.
" Awali Chama kilinisimamisha uenyekiti mwaka 2021 kwa tuhuma hiyo na tuhuma zingine za kupikwa ambazo hazikuwa na mashiko. Nilikwenda kulalamika kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya, Diana akasema ofisi haijapokea taarifa ya kuenguliwa kwa Mwenyekiti wa Kijiji na wajumbe waliochaguliwa na wananchi na kula kiapo.
"Mkurugenzi akanielekeza niendelee kufanya kazi na wajumbe waliosimamishwa hadi itakapoelekezwa vinginevyo na ofisi hiyo, sijakaa sawa mwaka jana mwezi Novemba Chama kikanisimamisha tena. Nashangaa tena Chama imeliibua upya jambo hilo wakati lilikuwa limeisha" anasema Magige.
Akizungumzia kuhusu kufungwa kwa kesi ya jinai amesema " Nilishtakiwa kwa kosa la kufanya fujo na kutishia kuua kwa maneno kesi ya 2020, dhidi ya wafanya usafi wa Kijiji jirani katika mpaka unaotenganisha Kijiji cha Magunga na Biatika kuhusu mgogoro wa mpaka wa vijiji hivyo.
"Nilihukumiwa kifungo cha nje cha miezi minne kwa makosa yote mawili kwasababu tu ya hila na chuki za watu, bado nimekuwa nikiandamwa, wenzangu waliokuwa wenyeviti wa Kijiji walionitangulia nao hawakumaliza muda wa uongozi walisimamishwa na chanzo ni Mwenyekiti wa CCM na Katibu CCM kata ya Mirwa ambao wanatanguliza mbele maslahi binafsi" anasema.
Kuhusu kukatalia kwenye eneo la Serikali (Daire) na kufanya makazi amesema " Mimi nilikuwa mtumishi wa Kampuni ya maziwa ya Daire iliyokuwa inanunua maziwa kwa wananchi inakusanya na kwenda kuuza, walijenga kituo cha kukusanyia maziwa nikatambulishwa Serikali ya kijiji kuwa mimi ndio mlinzi wao.
"Daire walinipa kazi ya ulinzi tangu 1988 baadae kampuni hiyo iliondoka nikiwa bado naidai pesa kama malipo ya ulinzi na hawakunipa taarifa kuwa wamehama, nilifuatilia mkoani kwenye ofisi zao nikaambiwa niendelee kulinda eneo lao kisha watanilipa.
"Baadae Kampuni hiyo ilibadilishwa sikujua walikokwenda, kwakuwa ni mali ya watu nilipewa kuilinda na hawakuwahi kuniandikia barua ya kuniachisha kazi bado nipo naendelea kulinda na hakukuwa na makabidhiano kuwa ni mali ya kijiji au ya Kampuni mi bado naendelea kulinda hadi watakaporudi wanipe malipo yangu niwaachie kituo chao.
"Kama eneo ni la kijiji na sio la Daire wao wawatafute waongee nao wanilipe malipo yangu ya ulinzi niwaachie jengo lao, mimi sijui kama ni eneo la kijiji au Daire maana mimi kazi yangu ilikuwa kulinda mali za Daire, eneo nimeliendeleza nimepanda miti ya mbao na matunda" anasema Magige.
Mtendaji wa Kijiji akacha kuzungumza
DIMA Online ikafika hadi ofisi ya Kijiji ili kuzungumza na Mtendaji wa Kijiji hicho Lucus Kagina lakini haikufanikiwa kumpata.Mwandishi wa chombo hiki cha habari akampigia simu ili kuzungumzia tuhuma za Mwenyekiti zilizoelekezwa kwake.
Pia kufahamu utata kuhusu eneo la Daire lakini hakuwa tayali kuzungumza kwani kila alipopigiwa simu alipokea na kisha kukata simu alipopigiwa tena alipokea na kusema betri la simu ni bovu kisha akakata simu.
Mmiliki wa Sheli azungumza
Washington Benasius ni mmiliki wa Sheli ya Mafuta ambaye pia ni Afisa Mifugo Kata ya Mirwa iliyopo kijijini hapo, anasema kwa taratibu za Serikali hakuna ushuru wa sheli ya Mafuta inayotolewa kwenye kijiji kwani wao tozo hulipwa Serikali kuu na Halmashauri.
Amesema hajavamia eneo la choo" sijavamia walilalamika hadi ofisi ya Waziri wa Afya, Watu wa Ardhi wa halmashauri walikuja wakapima ikaonekana vipimo vipo sawa kama alivyokabidhiwa na Serikali ya Kijiji.
" Mimi namiliki eneo kihalali, malalamiko yalipelekwa hadi Wizara ya afya yakafika kwa aliyekuwa Rais Hayati Magufuli uchunguzi ukafanywa na ikaonekana ni mmliki halali, sheli haitolewi ushuru kwenye kijiji, tunachokifanya ni kutoa huduma kwa jamii kama kujenga mahusiano.
" Mtendaji wa Kijiji ana taaifa yote ya vitu navyochangia kwenye kijiji, mfano ule ujenzi wa Zahanati nilichangia mchanga tripu saba, ujenzi wa tenki la maji shule ya msingi Magunga nilichangia mifuko ya saruji,nilitoa nondo wakati wakufunga lenta Zahanati, kuna barabara zilikuwa korofi nikapeleka greda barabara ikarekebishwa.
Anaongeza " Shule ya Msingi Kamimange nilipeleka mifuko mitano ya saruji,Soko la Magunga vibanda vilikuwa vya majamvi mimi ndiye nilihamasisha wakajenga vya bati na sasa wengine wana maduka, aliyehamasisha ujenzi wa choo sokoni ni mimi Washington likachimbwa shimo gari yangu ikasomba udongo na vibarua kwa gharama zangu.
"Daraja la Mirwa lilikatika mimi na Mwenyekiti wa Mirwa Ibrahim Aluma alituhamasisha kutengeneza barabara, tukahamasishana wadau wakajitokeza wakachangia nikatoa gari tukasomba mawe kwa gharama zangu daraja likapitika, pia nina gari linasaidia kusafirisha mihili ya Marehemu bure kwa familia zisizo na uwezo na wagonjwa wasio na uwezo.
"Kijiji cha Mirwa nimechangia saruji mifuko 10,wakati wa ujenzi wa ofisi ya kijiji na kupiga ripu ndani na nje,kuweka sakafu na kuweka milango kwenye vyumba 2 vya hiyo ofisi" anasema.
Afisa Mifugo huyo amekanusha kiwango cha ushuru wa mifugo kilichotwajwa na Mwenyekiti huyo nakusema ni uongo .
"Ng'ombe kwa siku wanachinjwa 2-3, mbuzi na kondoo kila siku ni wastani wa 10 isipokuwa siku ya mnada mbuzi na kondoo huchinjwa zaidi ya 20.
"Ushuru hukusanywa na vijana walioajiriwa na halmashauri, ng'ombe mmoja ni sh 2,500, mbuzi na kondoo ni 1,500,alichosema Mwenyekiti ni uongo nikutaka kuchonganisha wakusanya ushuru na Halmashauri ionekane wanahujumu mapato ya halmashauri" anasema Washington.
Amesema amekuwa akijitahidi kuchangamana na jamii katika kusaidia huduma mbalimbali na kumiliki sheli na amekuwa msimamizi mzuri wa makusanyo ya ushuru wa mifugo huku akijipongeza kwa uhamasishaji mzuri katika kuhaikisa bucha za nyama zinajengwa kwa ubora.
CCM Wilaya ya Butiama, Diwani wanasemaje kusimamishwa uongozi Magige Mahera? Endelea kufuatilia DIMA Online.
Gari zikiwa kwenye foleni zikisubiri abilia
Post a Comment