HEADER AD

HEADER AD

WANAWAKE WA WEJISA WAJIVUNIA UONGOZI WA RAIS SAMIA



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KAMPUNI ya Weka Jiji Safi (WEJISA Company Ltd) imepongeza juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya kufanya kazi ikiwemo wafanyakazi wanawake, jambo ambalo limeongeza uchapakazi.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo  Nuru Hassan amesema hayo kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yanayofanyika Machi 8 ya kila mwaka.


"Rais wetu Samia tunamuunga mkono kwa sababu nafasi aliyonayo amesaidia kuongeza mwamko kwa wanawake kufanya kazi na wale ambao walikua hawana kazi na kutafuta shughuli zozote ili waweze kujiondoa kwenye utegemezi," amesema Nuru.

Amesema kuwa, kampuni ya WEJISA  itaendelea kushirikiana na Serikali bega kwa bega na ndio sababu wameamua  kusheherekea pamoja na kujifunza mengi kwa wafanyakazi Wanawake.

Aidha, amesema kuwa amepata faraja kujumuika na Wanawake wenzake kwani wamekuwa chachu ya maendeleo ya Kampuni hiyo.

Wanawake hao wa WEJISA wanatoka vitengo mbalimbali ikiwemo wanaosafisha maeneo ya Jiji, ikiwemo ufagiaji, ukusanyaji wa taka na usafi wa mazingira.


Amesema lengo la tukio hilo ni kupeana moyo kama wanawake katika kuamua mambo ili kufanikisha utendaji bora wa kazi.

Naye Patricia Kimelemeta Mwandishi Kimara wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Mtoto mkoa wa Dar es Salaam, alitoa mada ya malezi na makuzi kwa watoto ambapo alitoa rai kwa wazazi kuendelea kutoa elimu kwa watoto wao ikiwemo kujenga ukaribu wa kuwachunguza ilikujua changamoto wanazokutana nazo.

Baadhi ya wanawake wafanyakazi wa WEJISA wameishukuru kampuni hiyo na kusema kuwa imekuwa mkombozi kwao na wamekuwa wakifanya kazi kwa moyo.


"Mie nina familia, nikitoka nyumbani naandaa kabisa chakula kwa wanangu ndiyo naenda kazini.

"Niwaombe wanawake wenzangu kuzingatia sheria za usalama barabarani kwani tumekuwa tukishuhudia matukio mengi, yakiwemo ya baadhi yao kugongwa.'  Amsema Asha Salum.


Sharifa Magombeka amesema kuwa, anafanya kazi ya kuzoa taka ilikupata kipato chake halali.

"Mwanamke ni kujitambua, nafanya kazi yangu ya kuzoa taka hii kupata kipato kihalali, tunamshuru Rais kuendelea kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji kazi, tumejumuika hapa tumepata elimu, lakini pia tumefurahi pamoja" amesema Sharifa.





No comments