HEADER AD

HEADER AD

DITOPILE AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEA KULIOMBEA TAIFA, RAIS SAMIA

Na Mwandishi Wetu, Kondoa

MBUNGE  wa Viti Maalum mkoa wa Dodoma Mariam Ditopile amewaomba wananchi na Viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa pamoja na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anapokuwa akitekeleza majukumu ya Taifa.

Ameyasema hayo wakati akigawa futari kwa Wazee, Wajane na Watu wasiojiweza katika wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma.


"Kwa imani yetu miezi yote ni bora lakini mwezi mtukufu wa ramadhani ni bora zaidi, na pia tunaambiwa katika mwezi huu dua yoyote utakayoiomba mbingu ziko wazi na Mwenyezi Mungu ametukumbusha kupitia suratul Insan aya ya 8 tuwafuturishe kile tunachokipenda".

"Sisi ni viongozi mmetuamini lakini juu yetu yupo Rais Dkt. Samia Suluhu Mwenyezi Mungu amempa majukumu ya kutuongoza, hata majukumu yake ya kifamilia ameyasahau kidogo na muda mwingi anahangaika na wananchi wa Kondoa, na kila mahali nchini.

"Anawaza leo nipeleke mradi wa maji wapi, leo nipeleke mradi wa umeme wapi, ni dhamira yake njema ya kuwatumikia watanzania, wapo wasioitakia mema Tanzania jukumu letu sote ni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu"amesema Mariam.

Ameongeza kusema kuwa ameamua kutumia mwezi huo wa ramadhani kuzunguka katika mkoa huo kutoa futari.


"Nimetumia mwezi huu wa Ramadhani kuzunguka mkoa wote wa Dodoma kufuturisha, nimeanza pale Dodoma mjini kwa kufuturu na yatima na wajane zaidi ya 300 na kisha kuwapa sadaka.

"Nimeshafuturisha wilaya za Bahi, Kongwa na leo nipo Kondoa. Pale Kongwa nilienda kijiji cha Mkoka pamoja na futari na nilienda kutembelea shule ya watoto wenye uhitaji maalum, ambako wapo watoto wadogo wenye ulemavu lakini walikuwa wamefunga, niwatakie ramadhani njema."amesema.
 


No comments