HEADER AD

HEADER AD

KONTENA LA VIFAA TIBA LILILOSUBIRIWA SIKU MBILI BILA MAFANIKIO KUWASILI LEO TARIME

Na Dinna Maningo, Tarime

MBUNGE wa Jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki amesema Gari lililobeba kontena lenye vifaa tiba lililotarajiwa kufika katika Hospitali ya wilaya Tarime April 26,2023
litawasiri leo April, 28,2023.

DIMA Online imezungumza na Mbunge huyo kupata uhakika wa lini gari lililodaiwa kusafirisha vifaa tiba litawasili Tarime kupeleka vifaa hivyo katika hospitali ya wilaya Tarime baada ya kusubiliwa kwa siku mbili bila mafanikio.

     Mbunge wa Jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki

"Gari limefika Makutano litaingia leo Tarime, nitatoa taarifa kamili likishawasili "amesema Kembaki.

Ni baada ya kusambaa matangazo kutoka ofisi ya mbunge huyo Katika mitandao ya kijamii yakiwemo makundi ya WhatsApp.

Tangazo hilo lilieza kuwa ofisi ya mbunge ina jambo lao muda wa saa 3: 00 kamili asubuhi katika hospitali ya wilaya ya Tarime April 26,2023 hivyo wananchi wajitokeze wafike katika hospitali hiyo kushuhudia jambo lao.
                             Tangazo

Katika mitandao hiyo ya kijamii zilisambazwa picha za gari lililodaiwa  kubeba vifaa tiba huku wananchi wakihamasishwa kujitokeza kushuhudia kontena hilo.

Hata hivyo ilipofika tarehe 26 wananchi wakiwemo wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) walifika hospitali na kukaa kwa saa kadhaa wakisubiri kontena la vifaa tiba lakini halikufika na hivyo kulazimika kuondoka.

Siku hiyo ya tarehe 26, 2023 majira ya jioni lilisambazwa tangazo lingine kwenye mitandao ya kijamii likieleza mabadiliko ya tarehe kuwa Kontena litawasili hospitali Aprili, 27,2023 ambapo haikuelezwa sababu ya konetana kutowasili tarehe 26.


Wananchi wanaccm walifika kushuhudia kontena na kulingojea kwa saa kadhaa bila mafanikio na kisha kufukuzwa na walinzi wa hospitali hali iliyowalazimu kuondoka katika viunga hivyo vya hospitali baada ya kusubiri bila mafanikio.

" Tulitangaziwa kwenye Magroup ya WhatsApp na mitaani kuwa mbunge katuletea vifaa tiba katika hospitali ya Bomani ambayo ni hospitali ya wilaya ya Tarime.

       Gari lililodaiwa kubeba vifaa tiba

" Wananchi na sisi makada wa CCM tulienda hospitali kushuhudia nimekaa pale masaa matatu tangu saa tatu asubuhi kama walivyotutangazia lakini hatukuona hilo kontena mi niliondoka zangu nikawaacha wengine wakiendelea kusubiri " amesema kada mmoja wa CCM.

Hata hivyo uongozi wa Hospitali hiyo ya wilaya ya Tarime ulipoulizwa kama unafahamu kuwasili kwa kontena la vifaa tiba uligoma kuzungumza na kudai wao sio wasemaji bali msemaji ni Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Tarime huku ukiomba aulizwe Mbunge wa Jimbo hilo.

Katibu wa mbunge wa Jimbo hilo Elisha Samo amesema" Nilikua nikifuatilia gari lililo na mzigo wa vifaa tiba, sasa tuko makutano kuja Tarime.

"Kesho saa tatu asubuhi wananchi wote tutakutana Hospitali Bomani na mh mbunge akikabidhi" amesema Elisha.

     Katibu wa mbunge wa Jimbo hilo Elisha Samo 




No comments