HEADER AD

HEADER AD

SIMAI AAHIDI KUTOA MILIONI 3 KILA GOLI LA SIMBA SC

Na Andrew Chale, Dar es Salaam

WAZIRI wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Simai Mohammed Said amekipongeza kikosi cha klabu ya Simba kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco huku akiahidi kutoa milioni 3 kwa kila goli la ushindi kwenye mchezo wa marudiano nchini Morocco.

Simai amesema hayo alipohudhulia mchuano huo katika mechi ya robo fainali ya Klubu Bingwa ya Afrika akishuhudia Jean Othos Baleke kuipatia Simba goli pekee la ushindi mpaka dakika 90 za mchezo huo uliochezwa  uwanja mkubwa wa Taifa wa Benjamin William Mkapa,Temeke Dar es Salaam. 

      Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar  Mhe. Simai Mohammed Said (mwenye kofia nyeupe) 

Simai amesema wizara yake katika kumuunga mkono Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan katika kushajihisha Utalii kupitia michezo, na yeye amewaahidi Wekundu hao Klabu ya Simba kuwapa Milioni tatu kwa kila goli katika mchezo wa pili wa marudiano huko Morocco. 

 "Kwa kweli Simba wameonesha kuwa Mabalozi wazuri katika kuitangaza Tanzania na Utalii wetu,
Juhudi zao ni vyema Watanzania kuziunga mkono, nitatoa motisha kwa kila goli," amesema Simai wakati wa tukio la utowaji wa pesa Milioni 5 za Rais Samia anazotoa kwa kila goli.




No comments