TET YAGAWA VISHIKWAMBI KWA WALIMU KIMBIJI
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KATIKA kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya elimu, TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) imechangia vifaa vya tehama kwa Walimu wa Shule ya Sekondari Kimbiji Dar es Salaam.
Pia imekabidhi vifaa vya Kielektroniki kupitia mradi wa KLIC 2022 (Korean e-learning Improvement Cooperation 2022)kutoka nchini Korea.
Zoezi hilo limeenda sambamba na ugawaji wa vyeti kwa Walimu 20 waliopata mafunzo ya tehama kwa kupata vishikwambi pamoja uzinduzi wa Maabara ya tehama shuleni hapo kupitia mradi huo wa KLIC 2022.
Akizungumza katika tukio hilo, Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk. Aneth Komba ameishukuru Serikali kuweka juhudi sekta ya elimu na mahusiano bora ya Kimataifa na Korea.
Mkrugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt.Aneth Komba Akizungumza katika tukio hilo la ukabidhaji wa vifaa vya kielektroniki vilivyotelewa na Korea kupitia mradi wa KLIC 2022 na uzinduzi wa Maabaraya TEHAMA.
"Naomba nimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, tunafahamu kwamba kupitia Wizara ya Elimu, walimu wote wamepata vishikwambi, na nina imani walimu hapa mnavyo vishikwambi.
"Kwa hiyo TET tumechangia kwenye juhudi za Rais wetu kwa kuongeza vishikwambi hivyo kwa lengo la kuhakikisha sasa kweli tunaenda kidijitali." Amesema Dk Aneth Komba.
Aidha, amewataka walimu hao kufundisha na kuongeza teknolojia katika manufaa bora ikiwemo kuwawezesha wanafunzi kupata fursa ya kutumia vifaa hivyo vya mradi wa KLIC 2022.
Mkrugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt.Aneth Komba Akizungumza katika tukio hilo la ukabidhaji wa vifaa vya kielektroniki vilivyotelewa na Korea kupitia mradi wa KLIC 2022 na uzinduzi wa Maabaraya TEHAMA.
"Tufundishe kwa njia zile za zamani za kitamaduni, lakini pia tukumbuke kuboresha ufundishaji wetu kwa njia bora ya kutumia vifaa vya tehama.
"Vifaa hivi vitasaidia utafutaji wa maarifa, watoto watumie vifaa hivi kuongeza maarifa yao, lakini pia TET inaomba kuhakikisha vinalindwa." Amesema Dk. Aneth Komba.
Ameongeza kuwa kwenye mitaala mipya elimu ya teknolojia imesisitizwa zaidi kwani inaandaliwa itakayowasaidia wanafunzi na kuwa bora zaidi.
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari kimbiji, Joseph Kiseke ameshukuru kwa uzinduliwaji wa maabara hiyo ya TEHAMA na kukabidhiwa vifaa vyote huku akieleza kuwa atahakikisha vinatumika ipasavyo katika kuboresha elimu.
Kwa upande wao baadhi ya walimu waliopatiwa vifaa hivyo vya tehama wamesema vitakuwa msaada kwao kwani vitawarahisishia katika kufundisha wanafunzi kwa urahisi.
KLIC 2022 ni programu ya mafunzo yaliyotolewa na nchi ya Korea kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa njia ya mtandao kwa Walimu 20 shule ya sekondari kimbiji.
Post a Comment