HEADER AD

HEADER AD

TET YAZINDUA MAABARA YA TEHAMA YAKABIDHI VIFAA VYA MRADI

Na Mwandishi Wetu, Dar  es Salaam

TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) imefanya uzinduzi wa Maabara ya TEHAMA kwa  shule ya Msingi Tegeta "A" ya jijini Dar es salaam sambamba na kukabidhi vifaa vya Kielektroniki kutoka nchini Korea kupitia mradi wa KLIC 2022 (Korean e-learning Improvement Cooperation 2022).

Makabidhiano hayo yamefanyika , Aprili , 18,2023. KLIC 2022 ni programu ya mafunzo yaliyotolewa na nchi ya Korea kwa  kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa njia ya mtandao kwa Walimu 20 wa shule ya Msingi Tegeta A.

Awali, Akikabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt.Aneth Komba amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha sekta ya Elimu nchini ambapo ameeleza kuwa walimu katika shule hiyo wataweza kutekeleza kwa urahisi kazi ya  ufundishaji na ujifunzaji kwa njia ya kieletroniki.

Mkrugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt.Aneth Komba Akizungumza katika tukio hilo la ukabidhaji wa vifaa vya kielektroniki vilivyotelewa na Korea kupitia mradi wa KLIC 2022 na uzinduziwaMaabaraya TEHAMA

Dkt Komba amewataka walimu hao kuhakikisha wanaleta matokeo chanya ambayo yatasaidia katika uboreshaji wa elimu.

"Mkayatumie mafunzo vizuri na vifaa hivyo mlivyokabidhiwa kwa kuleta matokeo chanya na tuone ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi wa Tegeta A", Amesema Dkt.Komba.

Tukio hilo liliambatana na kukabidhi vishikwambi 20 kwa walimu walioshiriki programu ya  mafunzo hayo.

Kwa upande wake , Mwalimu Mkuu wa shule ya Tegeta A, Alistides Ntakire ameshukuru kwa mafunzo hayo pamoja na vifaa vilivyotolewa ambapo amesema ana imani yataleta tija katika shule yake.

Mrugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt.Aneth Komba akikamkabidhi  Mwalimu Mkuu wa shule ya Tegeta A, Mwl. Alistides Ntakire vifaa vya kielektroniki vilivyotelewa na Korea kupitia mradi wa KLIC 2022. 

Nae Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo, Yassin Marijan ameshukuru kwa kuzinduliwa maabara hiyo ya TEHAMA  na kukabidhiwa vifaa vyote huku akieleza kuwa atahakikisha vinatumika ipasavyo katika kuboresha elimu.

Vifaa vilivyokabihiwa ni pamoja na 'UPS 26, computure Monitor 25, system Unit 25, Wirless keyboard 35, projector  moja, scanner moja, printer moja, wireless mouse 35, headphone 25, electric blackboard moja, webcamera 26, digital podium moja, wired keyboard 25,wired mouse 25, speaker 26, adapter 49 na usb flash disk 50'.

    Mkrugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt.Aneth Komba akiwa anavitoa kuwakabidhi vifaa vya kielektroniki vilivyotelewa na Korea kupitia mradi wa KLIC 2022 uongozi wa shule ya Tegeta A, kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mafunzo ya Mitaala, Dkt. Fika Mwakabungu. 

      Baaadhi Walimu wa shule ya Msingi Tegeta A,  wakiwa wamebeba vifaa vya kielektroniki vilivyotelewa na Korea kupitia mradi wa KLIC 2022.

     Mkrugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt.Aneth Komba akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Maabara ya TEHAMA katika shule ya Msingi Tegeta A, Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, Yassin Marjan. 

No comments