HEADER AD

HEADER AD

BUSTANI YA MBOGAMBOGA YAWAGOMBANISHA WANANCHI NA WALIMU


Na Mwandishi Wetu, Tarime

WANANCHI  na Walimu shule ya msingi Magena iliyopo kata ya Nkende halmashauri ya mji Tarime mkoani Mara, wameingia mgogoro kisa bustani ya mbogamboga ya walimu.

Imeelezwa kuwa mgogoro huo ni baada ya Walimu wa shule hiyo kuwazuia wananchi kuondoa miba waliyoizungushia kama uzio kwenye bustani ya mbogamboga ili wananchi wanaopita wasiweze kuzikanyaga lakini wakazing'oa. 

     Shule ya msingi Magena

Baadhi ya Wananchi wamedaiwa kukaidi na kuondoa uzio wakidai miiba imewekwa karibu na uwanja wa michezo wa mpira wa miguu wa shule hiyo ambao wanautumia kufanya mazoezi kila siku jioni.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Grace Guchaine amesema uharibifu huo wa mazao ya shule ulifanyika Mei, 23, 2023 usiku baada ya wananchi hao kukosa sehemu ya kufanyia mazoezi yao ya mpira wa miguu huku wakitoa vitisho vya kuchoma nyumba za watumishi wa shule waliojenga katika mitaa iliyoko karibu na shule.

         Bustani ya mbogamboga inayodaiwa kung'olewa na wananchi


"Walimu wameingiwa hofu kuwa watavamiwa wakati wowote na kudhuliwa, tayari nimetoa taarifa kwa mwenyekiti na mtendaji wa mtaa wa Shuleni na pia kwa mtendaji wa kata ya Nkende"amesema mwalimu mkuu wa shule hiyo.

Mwenyekiti wa mtaa wa Shuleni Mwenge Nyamohanga alipopewa taarifa hiyo amesema shule ndiyo imekosea kuwakataza wananchi kufanya mazoezi katika uwanja huo.

"Hawa ndio wanaochangia maendeleo ya shule kwanini wakatazwe kuchezea uwanjani hapo hadi magoli ya uwanja kung'olewa?" Amehoji Mwenge.

Watumishi hao wameiomba serikali kuwahamishia katika vituo vingine vya kazi ili kuwaachia wananchi shule wanayodai ni yao.

       Uzio kwenye bustani ya mbogamboga unaodaiwa kutolewa na wananchi

"Tuna shamba la migomba na mahindi kama miradi ya shule, lakini pia miti ya shule lakini wanaoingia mashambani kuvuna ndizi na mahindi watakavyo bila kujali kuwa ni kwa ajili ya uji wa watoto wao.

"Siyo hivyo tu hawashiriki kwenye maendeleo ya shule hii, choo kilijaa  tangu 2018 lakini wameshindwa kukijenga wakidai ni kazi ya Serikali," amesema mmoja wa walimu katika shule hiyo.


No comments