HEADER AD

HEADER AD

KAMPUNI YA ORYX GAS YATANGAZA NEEMA KWA WATEJA


Na Boniface Gideon, Tanga

KAMPUNI ya uuzaji na usambazaji wa mitungi ya GAS ORYX mkoani Tanga  imefanikiwa kufikisha huduma ya matumizi ya gesi kwa wananchi waishio pembezoni na vijijini ikiwa ni mkakati wao wa kuhakikisha wanamfikia kila mmoja.

Pia kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupiga vita matumizi ya mkaa na kuni katika shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupikia.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya kumi ya biashara na viwanda yanayofanyika mkoani  Tanga, Afisa  masoko Andrew Noel amesema pomoja na kufanikiwa kufikisha huduma hiyo katika maeneo ya vijijini bado wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya nishati mbadala.

     Afisa masoko Kampuni ya uuzaji na usambazaji wa mitungi ya GAS ORYX,Andrew Noel

Amesema lengo ni kuhakikisha wanawasaidia ili kuondokana na adha ambazo zinaweza kujitokeza pindi wanapoendelea kuitumia.

Andrew amesema kuwa kwa kupitia maonyesho ya biaashara yanayofanyika kila mwaka mkoani Tanga ambayo hukusanya makampuni , taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali kwa lengo la kutangaza biashara na huduma wanazo zitoa kwa jamii, ni fursa ya kipekee  kwao kuzidi kuwafikia wateja mbalimbali kwa njia ya elimu wanayoitoa kwa wanaofika katika maonyesho hayo.

“Kama Oryx gas tunajivunia katika huduma zetu na tumeweza kuwafikia wateja wetu mpaka wa vijijini kabisa  ambao wapo ndani, tuligawa mitungi zaidi ya 600.

" Huu ni mkakati ambao tulijaribu kumsaidia mwanamke ambaye anafanya biashara za ujasiriamali ili kumsaidia katika kuokoa muda wa kufanya baiashara zake”amesema Andrew.

Ameongeza kuwa Oryx Gas inaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kupinga matumizi ya kuni  na mkaa kwaaajili ya kupikia ambapo huchangia kwa kiasi  kikubwa athari za mabadiliko ya tabia nchi kutokana na ukataji wa miti hovyo.
        Afisa Masoko akitoa elimu kwa mwananchi ya matumizi ya gas

“Tunatoa elimu kwa wateja wetu hasa hasa ya usalama na kuwahimiza wananchi na wateja mbalimbali ambao  bado hawajaanza kutumia nishati ya gas waanze kuitumia.

"Mkaa na kuni watu wengi kwa sasa wanaamini kwamba ni nishati ya bei rahisi sana ambayo inawasaidia katika matumizi lakini kiuhalisia nishati ya kuni na gas katika gharama nishati ya gas ni rahisi zaidi kuliko kuni na mkaa” amesema Andrew.

Ameongeza “Madhara mbayo yanasababishwa na kuni na mkaa yako mengi na mengi zaidi yanaingia katika mfumo wa mapafu na upumuaji, kwa kuangalia kwa karibu unaweza ukajihisi uko salama lakini baadaye wengi wanajikuta wana matatizo mbalimbali.

" Hii yote inatokana na matumizi ya kuni na mkaa. Niwasihi sana wananchi tuachane na matumizi ya kuni na mkaa tuhamie kwenye gas mbadala kwa matumizi mbalimbali ili kuondokana na mabadiliko ya tabaia nchi”amesema.

Maonyesho ya biashara hufanyika kila mwaka jijini Tanga yakihusisha makampuni na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali ambapo kwa mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu ya ‘Kilimo , viwanda utalii na madini ndio msingi wa maendeleo ya kiuchumi’.


No comments