RAIS SAMIA AMUONDOA U-RC MEJA JENERALI MZEE
>>Ma -RC wengine wahamishwa Mikoa
>>Kihongosi wa UVCCM apata shavu U-DC
Na DIMA Online, Dodoma
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya baadhi ya wakuu wa Mikoa, uteuzi wa wakuu wa mikoa, uhamisho wa wakuu wa Mikoa na uteuzi wa mkuu wa Wilaya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan
Kwa mujibu wa Taarifa kwa vyombo vya Habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus, imeeleza kuwa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Urambo mkoani Tabora Said Mohamed Mtanda ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mara.
Mtanda amechukua nafasi ya mkuu wa mkoa wa Mara Meja Jenerali Mzee Mungiya Mzee ambaye atapangiwa majukumu mengine.
Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Rukwa Queen Cuthbert Sendiga amehamishwa kuwa mkuu wa mkoa wa Manyara huku aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Manyara, Charles Makongoro Nyerere amehamishwa kuwa mkuu wa mkoa wa Rukwa.
Wakati huo huo,Rais Samia amemteua Katibu mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi kuwa mkuu wa wilaya ya Urambo akichukua nafasi ya Mtanda ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mara.
Mabadiliko, uhamisho na uteuzi huo umeanza mara moja. Uapisho wa mkuu mpya wa mkoa wa Mara utafanyika tarehe 24, Mei, 2023 saa 10:00 jioni Ikulu Chamwino.
Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee
Said Mohamed Mtanda
Charles Makongoro Nyerere
Post a Comment