SELF MICROFINANCE FUND YAWAKARIBISHA WANANCHI WENYE SIFA KUCHANGAMKIA MIKOPO
Na Mwandishi Wetu, Tanga
TAASISI ya Mfuko wa Self Microfinance inayojihusisha na ukopeshaji wa fedha imefanikiwa kuyagusa makundi mbalimbali na shughuli wanazozifanya wananchi hii ikiwa na lengo la kuwawezesha kujikwamua kiuchumi pale ambapo taasisi na mtu binafsi atahitaji kujiendeleza ili kupata faida zaidi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika maonyesho ya biashara na utalii yanayofanyika kila mwaka mkoani Tanga, Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Self Microfinance Julius Mungengele amesema lengo la taasisi hiyo ni kumfikia kila mteja kulingana na shughuli anayoifanya, taasisi na watu binafsi wenye vigezo ya kuweza kupata mikopo hiyo yenye riba nafuu pale ambapo watajiridhisha mteja wao anakidhi kupata mikopo wanayotoa.
" Lengo kuu la kutoa mkopo ni kumsaidia, tunataka aonyeshe nia kweli ya kutaka kubadilika na sisi riba yetu ni nafuu na rafiki kwa mteja, cha kusistiza tu ni kwamba lazima mteja azingatie vigezo na masharti ikiwemo muda wa mkopo wake"amesema.
Julius amezitaja huduma wanazotoa kwa wateja wao ni pamoja na mikopo ya kilimo , mkopo wa mkulima, biashara , Imarika, amtaji, mkopo wa mshahara ambazo wanazitoa kwa riba nafuu kwa wanufaika wao.
"Miongoni mwa huduma ambazo Self Microfinance finance tunazitoa na zimewanufaisha wateja wetu na zimegusa zaidi jamii ya watu wa hali ya chini ni mkopo wa mkulima, mkopo wa kilimo na mtaji lakini pia tunatoa mikopo hii kwa riba nafuu hasa ya mshabara, biashara na mkopo wa Imarika" amesema .
Aidha amewataka wananchi hususani wenye sifa za mikopo zikiwemo wadhamini, mali inayodhaminika ,leseni za biashara na vitambulisho vinavyomtambulisha mnufaika kufika katika mabanda hasa kipindi hiki cha maonyesho ya baishara na utalii yanayoendelea katika viwanja vya Mwahako ili kupata elimu zaidi.
Pamoja na hayo amesema mfuko wa Self Microfinance unaendelea kutoa elimu kwa wananchi katika kujiendeleza kiuchumi kupitia sekta ya kilimo biashara huku akiwataka kuchangamkia fursa zinazopatikana ili kuweza kujiletea maendeleo.
Maonyesho ya biashara na utalii yanayofanyika mkoani Tanga ambayo ni ya 10 mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu isemayo ‘Kilimo , 'Viwanda Utalii na Madini ndio msingi wa maendeleo ya kiuchumi’.
Post a Comment