HEADER AD

HEADER AD

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUFANYA KAZI BILA UPENDELEO

 

Na Alodia Babara, Bukoba

WAANDISHI wa habari mkoani Kagera wametakiwa kufanya kazi kwa weledi,kufuata maadili ya uandishi wa habari bila upendeleo na kutoshinikizwa na mtu yoyote ili kuandika habari za uongo zitakazohatarisha amani ya nchi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Siima katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani yaliyofanyika kimkoa mjini Bukoba, Mei, 20,2023 ambapo kidunia uadhinishwa kila mwaka ya Mei, 3.

      Mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Siima aliyesimama akizungumza katika maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Kagera yaliyofanyika ukumbi wa Bukoba Coop

"Kubalance ni wajibu wa mwandishi kufuatilia pande zote mbili, mfano kunapokuwepo malalamiko kutoka pande zote, pale unapolazimishwa useme hivi kwamba utalipwa kitu fulani lakini unajua unachosema siyo sahihi, hivyo timizeni majukumu yenu kwa weledi mliousomea na mlionao"amesema.

Siima amesema waandishi wa habari wa mkoa wa Kagera wamekuwa kichocheo cha maendeleo ya mkoa huo ndani na nje kutokana na kuandika habari za kuutangaza vyema huku akiwashauri waendelee kutoa ushirikiano huo.

Ameahidi kwamba Serikali ya Wilaya itaendelea kushirikiana nao ili kuleta maendeleo makubwa .

Kwa upande wa mwezeshaji Peter Matete ambaye ni mwenyekiti wa chama cha mawakili wa kujitegemea mkoani Kagera (TLS) alidadavua juu ya kauli mbiu ya siku hiyo ambapo amesema kuwa mtu yoyote kama hajasikilizwa anakuwa amenyimwa haki ya msingi ya mwanadamu ambayo anapaswa kuipata tangu anapozaliwa .

   Waandishi wa habari Mkoani Kagera wakiwa kwenye picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Siima

Naye mwenyekiti wa KPC Mbeki Mbeki amewashauri waandishi kufanya kazi kwa kufuata misingi mikuu ya mwandishi wa habari ambayo ni mustakabali wa haki.

Naye mdau wa habari ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika mkoani humo (KCU 1990) Respicius John amewaomba waandishi wa habari kama wadau muhimu kuendelea kuelimisha wananchi hasa wakati wa kuelekea kwenye msimu wa 2023/2024 katika kutunza ubora wa zao la kahawa ili waweze kupata bei kubwa na kunufaika nalo kwa kujiongezea kipato na Taifa kwa ujumla.




No comments