WADAU WAOMBWA KUCHANGIA FEDHA LIGI YA MPIRA WA KIKAPU MARA
>>Ili kufanikisha ligi hiyo inahitajika Tsh. Milioni 21
>>Fedha zilizopatikana ni Tsh. 8,945,000
Na Dinna Maningo, Tarime
CHAMA cha Mpira wa Kikapu (Basketball) mkoa wa Mara (MARBA) kinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa fedha kwa ajili ya kuendesha ligi ya mpira wa kikapu inayofanyika kimkoa katika chuo cha ualimu wilayani Tarime.
Ligi hiyo ya mkoa imeanza Mei, 07, 2023 na inatarajiwa kukamilika Julai, 22,2023 ambapo vilabu saba vikiwemo vya wanaume na wanawake vimeshiriki ligi hiyo licha ya ukata unaovikumba.
Mwenyekiti wa mpira wa miguu mkoa wa Mara ambaye pia ni afisa kilimo Halmashauri ya wilaya ya Tarime, Sylvanus Gwiboha amesema katika makadilio ligi inahitaji jumla ya Tsh. 21,000,000 ili iweze kufikia malengo yake.
Mwenyekiti wa mpira wa miguu mkoa wa Mara ambaye pia ni afisa kilimo Halmashauri ya wilaya ya Tarime, Sylvanus Gwiboha akizungumza wakati wa uzinduzi wa ligi ya mpira wa kikapu
" Nachukua fursa hii kushukuru mgodi wa dhahabu wa North Mara, Vilabu shirikishi, wadau binafsi ambao wameitikia na kuchangia ligi na hivyo kupata jumla Tsh. 8,945,000, tunapungukiwa kiasi cha Tsh. 12,055,000, chama kinakaribisha wadau kuchangia.
Mwenyekiti huyo amesema timu zilizoshiriki zipo 7 kati ya hizo za wanaume 4 wanawake 3. Wilaya zenye timu ni Tarime timu 3 kati ya hizo moja ni ya wanawake na Musoma timu nne kati ya hizo mbili ni za wanawake
" Timu kutoka Tarime ni North Mara, Young vita na women Tigress, za Musoma ni Mwembeni, Fox , Tanesco na Divas." amesema Gwiboha.
Mwenyekiti huyo amewashukuru viongozi wa vilabu kwa kukamilisha zoezi la usajili kwenye mfumo wa TBfmap kwa vilabu kulipia ada ya usajili.
" Tumefanikiwa kusajili vilabu saba ambavyo vinashiriki ligi ya mkoa, tunawashukuru vilabu kwa michango yao wakati wadau wengine wakijipanga" amesema.
Akieleza historia ya mpira wa kikapu Mwenyekiti huyo amesema kuwa, Chama cha Mpira mkoa wa Mara kilianzishwa Septemba, 14, 2023 na kusajiliwa na Baraza la michezo Tanzania (BMT).
Amesema chama kimepewa mamlaka ya kukuza, kusimamia mpira wa kikapu mkoani Mara na shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF) lakini pia ni mwanachama wa shirikishisho la mpira wa kikapu Tanzania.
"Kwa kufuata kalenda ya TBF tumeandaa ligi ya mkoa wa Mara kwa mwaka wa pili, mwaka jana ligi ilifanyika kwa kushirikisha timu za mpira wa kikapu kutoka wilaya ya Bunda, Musoma na Tarime.
" Ligi ilipitia changamoto nyingi mwaka jana ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mdhamini wa uhakika, michango mingi ilitoka kwa viongozi pamoja na wadau wachache.
Amewashukuru wadau waliojitikeza kwa michango yao ya hali na mali kwaajili ya kufanikisha ligi ya mwaka jana ambayo ilikuwa ni kwa mara ya kwanza kwa mkoa wa Mara kuwa na ligi ya kimkoa.
Waliovaa jezi nyeupe ni timu ya wanawake Women Tigress ya Tarime na timu ya TANESCO ya Musoma wakishindana wakati wa uzinduzi wa mpira wa kikapu Mei, 28,2023
Waliovaa jezi ya njano mchanganyiko na bluu ni timu Mwembeni kutoka Musoma na timu ya North Mara ya Tarime wakishindana wakati wa uzinduzi
Post a Comment