FILAMU YA ‘MARRIED TO WORK’ KUFUNGUA PAZIA TAMASHA LA ZIFF
Na Andrew Chale, Dar es Salaam
FILAMU ya Married to Work iliyowahusisha wasanii wa ndani na wa je, akiwemo Idris Sultan, inatarajiwa kufungua pazia la tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF).
Tamasha hilo litafanyika jioni ya Juni 24, 2023, katika viunga vya Ngome Kongwe, Unguja, Zanzibar ambapo mwaka huu ni wa msimu wa 26.
Mtendaji Mkuu wa Tamasha hilo la ZIFF, Prof. Martini Mhando ametangazia Umma juu ya utambulisho wa kuanza rasmi wa tamasha hilo siku ya Juni 24, ambapo amewaomba wadau wakiwemo wasanii wa filamu wakongwe na chipukizi pamoja na watu wa ndani na nje kujitokeza kwa wingi kushuhudia filamu uzinduzi huo pamoja na filamu mbalimbali, kuanzia Juni 24 hadi Julai 2, mwaka huu.
“Juni 24 ndiyo itakuwa siku ya kufungua tamasha ‘Married To Work’, inayohusisha vituko vya wapendanao lakini ikiwa na mambo kadhaa yanayohusu Tanzania licha ya kufanywa na mtu kutoka nje.
"Mambo hayo ni kuionyesha Zanzibar kama kisiwa cha ajabu cha mapenzi na ndoto, lakini pia kutakuwa na waigizaji wa Tanzania kimataifa ukiiona utaelewa kwa nini Ziff waliona inafaa kuzindua msimu wa 26 wa tamasha hilo,”amesema Prof. Mhando.
Aidha, amesema tamasha hilo, linatarajiwa kukusanya wageni zaidi ya 200,000 visiwani Unguja wakati wa tamasha na kwamba linaenda kuiongezea tija katika kuhakikisha uchumi wa bluu na Utalii.
Prof. Mhando amsema kabla ya tamasha hilo walipokea filamu 3,000 kutoka kila kona ya dunia, huku zilizotoka Afrika Mashariki zikiwa 206 na filamu kutoka Tanzania pekee zikiwa 64 huku Zanzibar zikiwa 12 na filamu mbili pekee zilionekana bora kushinda nyingine na kupitishwa.
Baadhi ya filamu nyingine zitakazoonesha ni pamoja na;
Upande wa filamu ndefu ni; Bounty (Switzerland), L.I.F.E. (Nigeria), Twin Flame (Usa/Nigeria), Wandongwa (Tanzania), Still Okay To Date? (Tanzania)Soudabeh (Iran), Citizen Kwame (Rwanda) When The Levees Broke (Cameroon),Wounded Psyche (Iran),Mister Sister (Canada-Usa) na Dodoma (Tanzania).
Zingine ni; Gereza (South Africa), Behind Gates (Cameroon), Half Open Window (Kenya)
Eoni2023(Tanzania) na Karmanye (India).
Kwa upande wa filamu fupifupi; An Irish Goodbye (Ireland), Deep (South Korea), The Mist (South Korea), Moksa’s Freedom (Indonesia), Kitendawili (Tanzania), Sweta (Tanzania),One Day Plus Eternity (Iran), Jasiri (Tanzania),Hummus And Chips (Egypt), Flesh And Blood (Tunisia),Light Blue (Egypt).
Pia zipo; Re-Casted (Iraq), Cobbler Of Paradise (Iraq),Neb Tawy (Egypt), The Moped And The Goldfinch (Algeria),Na Zongi (Angola),9 Memeza (South Africa), Epiphany (United States), Under The Bed/Chini Ya Chaga (Tanzania), Ziwa (Uganda), Laila (Saudi Arabia), The Shoes That Get Smaller Every Night (Bahrain).
Fraiha (Qatar), Laugh Lines (Bangladesh), Act Of Love (Kenya), Seven Stages (South Africa), Supastaz (Kenya), A Beautiful Mess (South Africa), Talk To Me (Kenya),The Broken Mask (Nigeria), In The Stillness (Nigeria), A Void Life (Uganda).
Zingine ni Our Territories, Our Voice (Kenya), Ngozi Nyeusi (Tanzania), I Believe In Me (Tanzania),Nia (Tanzania), Little Egret (Egypt), Oleander (South Africa), My Girlfriend (Egypt), Clouded (South Africa), Mwandishi /Writer (Tanzania), Mawimbi (Kenya) na Katope (Tanzania).
Wadhamini wa tamasha hilo ni pamoja na Umoja wa Ulaya [EU], Ubalozi wa Switzerland Tanzania, na Shirika la GIZ. “Zanzibar ni njema, atakaye naaje”.
Post a Comment