ZAIDI YA BILIONI 822 ZA TARURA KUNUFAISHA WANANCHI MRADI WA RISE
Na Mwandishi Wetu, Iringa
WANANCHI katika Mikoa ya Iringa, Tanga, Lindi na Geita wanatarajiwa kunufaika na Mradi wa Uboreshaji wa Barabara Vijijini kwa ushirikishaji wa jamii na ufunguaji wa fursa za kijamii na kiuchumi (RISE).
Zaidi ya Tsh. Bilioni 822 zitatumika kuboresha miundombinu ya barabara vijijini.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi na usimamizi baina ya TARURA na wakandarasi wa ujenzi na usimamizi wa mradi wa RISE iliyofanyika mkoani Iringa, waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Angela Kairuki (Mb), amesema;
" Mradi huo wa RISE unaenda kuwakomboa wananchi hasa waishio vijijini kwa kuwafungulia fursa za kijamii na kiuchumi.
“Asilimia kubwa ya watanzania tunaishi vijijini na ndiyo kwenye changamoto kubwa sana za miundombinu zilikuwa zinaleta athari kubwa sana za kiuchumi na kijamii ikiwemo kukosa huduma za msingi za kijamii na kuchangia umaskini" amesema.
Ameongeza "Tumeshuhudia mazao yakiozea mashambani na mengine barabarani. Mradi huu sasa unaenda kuleta taswira mpya kabisa kwa maeneo hayo ya vijijini.
"Nimefurahia zaidi kuona sasa mradi huu unaenda kugusa mazao ya chai, matunda kama parachichi na mazao ya misitu na ndiyo maana uliasisiwa,” amesema Kairuki.
Aidha Kairuki amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita kupitia TARURA imekuwa ikifanya jitihada za dhati kuhakikisha kuwa inaboresha barabara za vijijini ili ziweze kupitika.
Amesema tangu Dkt. Samia Suluhu Hassan aingie madarakani bajeti ya TARURA imeongezeka kwa takribani mara tatu toka Tsh. Bilioni 200 mwaka 2021 hadi Bilioni 836 kwa mwaka 2023/2024.
“TARURA sasa mjipange kikamilifu na mhakikishe kuwa mnasimamia wakandarasi kwa karibu ili kazi zifanyika kwa ubora wa hali ya juu na kwa wakati ili kufikia malengo yanayotarajiwa. Pia mhakikishe wananchi wanapewa fidia stahiki na kwa wakati,” amesema Kairuki.
Amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuendelea kuwajali watanzania hasa wa hali ya chini na kueleza kuwa hawana cha kumlipa bali wananchi waendelee kumuunga mkono kwa hali na mali ili aendelee kuwatumikia,” amesema Mhe. Kairuki.
Kwa upande wake Mtendaji mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff amesema kuwa lengo la mradi wa RISE ni kuboresha barabara za vijijini.
Pia kutoa fursa za ajira kwa wananchi katika maeneo ya vijijini yaliyochaguliwa na kujenga uwezo wa kitaasisi katika usimamizi endelevu wa barabara za vijijini kwa kutumia mbinu za ushirikishwaji wa jamii.
“Mradi huu utashirikisha jamii zinazoishi kandokando ya barabara katika kazi za matengenezo ya kawaida na kupatiwa mafunzo chini ya mradi,” amesema Mhandisi Seff.
Naye Mbunge wa Jimbo la Mafinga Kaskazini Mhe. Exaud Kigahe ambaye pia ni Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, amesema kuwa mradi huo utawanufaisha wananchi kwa kuleta uzalishaji wenye tija na unafuu wa kusafirisha pembejeo na mazao kutoka shambani kwenda viwandani na kwenye masoko.
Mradi huu pia utavutia wawekezaji kwa sababu ya ubora wa barabara zitakazojengwa, viwanda vingi vitajengwa katika sekta ya misitu na kilimo ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani ya mazao.
Hakika Dkt. Samia Suluhu Hassan tumpe maua yake kwa kutujali na kutukomboa wananchi wa Mtili, Ifwagi na Wenda-Mgamakwani kwa mara ya kwanza tunaenda kupata lami,” alisema Kigahe. wa RISE unatarajiwa kujenga kwa kiwango cha lami kilometa 535 za barabara vijijini ambapo kilometa 400 zitajengwa na TARURA na kilometa 135.
Zitajengwa na TANROAD katika wilaya za Iringa, Mufindi na Kilolo mkoani Iringa; wilaya ya Handeini mkoani Tanga; wilaya ya Mbogwe mkoani Geita; na wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
Post a Comment