HEADER AD

HEADER AD

MWENYEKITI CCM AWATAKA WAHIFADHI KUWATUMIA WANASIASA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII



Na Boniface Gideon, Pangani

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tanga, Rajabu Abdarahman ameelezea kuridhishwa kwake na hatua ya Wahifadhi kuhitaji kuwatumia wanasiasa hususani wale wa kutoka Chama tawala katika kuitangaza Sekta ya utalii ili kuongeza tija sekta ya Utalii.

Rajabu ameyasema hayo Juni, 20, 2023, ikiwa ni muda mfupi baada ya kukutana na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere  Ephraim Mwangomo ambaye alimzawadia kitabu maalum cha kutunza Kumbukumbu kama ishara ya kuimarisha ushirikiano. 

Rajabu amesema atawajibika kutumia nafasi yake kupitia majukwaa ya siasa kuhamasisha wananchi kutembelea hifadhi zilizopo kwenye maeneo yanayowazunguka kwa vile Utalii siyo kwa ajili ya wageni kutoka nje pekee.

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tanga, Rajabu Abdarahman

Kwa upande wake Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere Ephraim Mwangomo amesema, wahifadhi wamejipanga kushirikiana na viongozi mbalimbali hasa wanasiasa wanaoishi maeneo yenye vivutio vya utalii ili kusaidia kufikisha ujumbe juu ya suala la uhifadhi.

     Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere Ephraim Mwangomo

Mbali na hayo, Kamishina Mwangomo amesema  kuwa ushirikiano huo pia utasaidia kutangaza utalii akisisitiza kusema kwamba iwapo watu wote watazungumza lugha moja itawezesha kukuza sekta hiyo ya utalii hapa nchini. 

No comments