HEADER AD

HEADER AD

TRA YAPOKEA MAONI YA WADAU WA SEKTA YA UTALII


Na Andrew Charle, Arusha

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema inapokea maoni ya wadau wa sekta ya utalii katika masuala ya utozaji wa kodi ili kuimalisha uchumi wa nchi kwani sekta hiyo ni sekta muhimu nchini.
 
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi, Richard Kayombo ameyasema hayo Jijini hapa katika maonesho ya Utalii ya Karibu Kill Fair yaliyoanza leo Juni 2-4, mwaka huu katika viwanja vya Magereza, Kisongo Arusha.

      Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi, Richard Kayombo (wa pili kulia) akizungumza na mgeni rasmi Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar (aliyevaa suti nyeusi) Simai Mohammed Said

‘’TRA kwa kushirikiana na Mameneja wetu wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini, Meneja wa Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja na Meneja wa Tanga, tupo hapa kwa lengo kuu la kushirikiana na wadau wetu wa sekta ya Utalii kueleweshana na wahusika kulipa kodi kwa wakati na kwa utaratibu wa kisheria’’ amesema Kayombo.
 
Ameongeza kuwa, wanapokea maoni ya wadau hao wa sekta ya Utalii kwani imekuwa ni miongoni mwa sekta kubwa inayobeba sekta nyingi ndani yake.

Amesema wanaamini nchi ikishindwa kukusanya mpato yake vizuri itakosa miundombinu mizuri na watalii watashindwa kutembelea. Hivyo wanatoa elimu sahihi na kupokea maoni kuona namna bora ya ulipaji kodi.

 Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi, Richard Kayombo 

‘’Tunatambua sekta ya utalii, inagusa sekta ya anga, usafiri wa ardhini, hoteli, matumizi ya mafuta, na matumizi mengine, hivyo tunatambua Utalii ukiwa imara, na sekta zingine zote zitasimama imara, ila sekta ya utalii ikiporomoka zingine zitaumia na Serikali itakosa mapato.

"Serikali ikikosa fursa ya mapato na miundombinu itashindwa kujengwa na maeneo mengine yatakosa fursa kutokana na kutofikiwa kwa watalii.’’ amesema Kayombo.
 
Kayombo ameongeza kuwa, wanatumia maonesho hayo kwa siku zote za maonesho na huduma zingine zitaendelea ikiwemo elimu kwa mlipa kodi.
  
Aidha, amesema kuwa, utalii kanda ya kaskazini ni mwakilishi wa utalii kanda zote za Tanzania Bara, huku pia utalii ukiwa katika Visiwa vya Zanzibar. 

No comments