HEADER AD

HEADER AD

WAANDISHI WA HABARI WASHAURIWA KUANDIKA HABARI ZA KUELIMISHA JAMII


Na Alodia Babara, Karagwe

WAANDISHI wa habari mkoani Kagera wameshauriwa kuandika habari zinazoelimisha jamii kutowanyanyapaa na kuwabagua wahanga wa virusi vya ugonjwa wa marburg baada ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kusema kuwa ugonjwa huo umeisha.

Ushauri huo umetolewa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Agnes Mwaifuge wakati akitoa mafunzo kwa Waandishi wa Habari mkoani humo ya kupinga unyanyapaa na ubaguzi kwa wahanga hao na familia zao.

      Mganga mkuu halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Agines Mwaifuge akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoani Kagera.

Mafunzo hayo yametolewa na Radio Karagwe kwa kushirikiana na mtandao wa Radio za kijamii chini ya ufadhili wa shirika la kimataifa la kuhudumia watoto duniani (UNICEF).

"Tuandike habari zinazoelimisha jamii na kuwatia moyo famila za wahanga wa Marburg watambue kwamba huo ni ugonjwa kama yalivyo mengine tusiwanyanyapae kwani tukiwabagua inaweza kusababisha madhara kama vile kuwajengea hofu, kuwakatisha tamaa, kujiona kuwa wao hawafai na kujiua" ameeleza Mwaifuge.

Anasema kutowabagua wagonjwa wa magonjwa yoyote yanapotokea katika jamii hususani ya mlipuko itasaidia watu kutoa taarifa, kupima, kupata matibabu, kupunguza maambukizi na kuwa huru.

Pia amewashuri kuandika habari ambazo hazitaleta taaruki kwa jamii pale wanaporipoti habari za mlipuko wa ugonjwa fulani na kuhakilisha wanajiridhisha kwa wahusika.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Radio Karagwe mchungaji Godfrey Aligawesa akifungua mafunzo hayo ya siku moja amesema licha ya kutoa mafunzo kwa Waandishi wa habari pia watafika maeneo mbalimbali mkoani hapo.

Maeneo watakayotembelea ni kwenye mikusanyiko ya watu kama kwenye minada ya n'gombe, mipakani, kata za Kanyangereko na Maruku kwa ajili ya kuelimisha jamii kuhusu hasara za unyanyapaa na ubaguzi kwa wahanga wa ugonjwa wa Marburg. 

Ikumbukwe kuwa ugonjwa wa Marburg ulitangazwa rasmi hapa nchini na Waziri wa afya Ummy Mwalimu Machi 19,2023 na kukoma rasmi Juni 02,2023 baada ya wataalam wa afya kujiridhisha kuwa hakuna maambukizi mapya.

No comments