HEADER AD

HEADER AD

WAGONJWA 87 HOSPITALI YA MUHIMBILI- MLOGANZILA WAWEKEWA PUTO

Na Andrew Charles, Dar es Salaam

HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili-Mloganzila imeendelea kuboresha huduma zake za kibingwa ya kibobezi ambapo hadi sasa imeweza kuwawekea puto (Intragastric ballon) wagonjwa 87, tokea kuanza kwa huduma hiyo hivi karibuni hapa nchini. 

Hayo yameelezwa Juni, 15, 2023 na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha hali ya Uchumi wa Taifa ya mwaka 2022 na mpango wa maendeleo wa Taifa wa mwaka 2023/24 upande wa sekta ya afya Bungeni mjini Dodoma. 

    Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba

Pia amesema ujenzi wa kituo cha upandikizaji viungo na ukarabati wa wodi za watoto mahututi (NICU) umekamilika katika  hospitali hiyo ya Taifa. 

Waziri huyo amesema Serikali imeendelea kuboresha huduma hizo nchini kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wake ambapo jumla ya wagonjwa 25 wamepatiwa huduma ya upandikizaji wa uroto katika hospitali za Muhimbili na Benjamin Mkapa. 

"Upatikanaji wa huduma hii hapa nchini umepunguza gharama za kupata huduma nje ya nchi kutoka Tsh. Milioni 250 hadi kufikia Tsh. Milioni 70 sawa na punguzo la asilimia 72 ya gharama" amesema Dkt. Mwigulu. 

Aidha, Dkt. Mwigulu amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya kielelezo na ya kimkakati, kuimarisha sekta za uzalishaji ili kutoa mchango katika ukuaji wa uchumi, kufungua fursa zaidi za ajira na maendeleo ya watu, kuboresha upatikanaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi zikiwemo huduma za afya.


No comments