BENKI YA TCB YAKABIDHI SARUJI MIFUKO 100, MABATI 100 SHULE YA MASIWANI
Na Boniface Gideon, Tanga
BENKI ya Taifa ya Biashara TCB( Tanzania Commercial Bank) imekabidhi vifaa vya vya ujenzi katika shule ya msingi Masiwani iliyopo kata ya Majengo Jijini Tanga.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa Julai,18,2023 ambavyo ni pamoja na Mifuko ya Saruji 100 na Mabati 100 kwaajili ya kuezekea .
Akikabidhi msaada huo Meneja wa Benki hiyo Tawi la Tanga Patrick Swenya amesema msaada huo ni sehemu ya kurejesha fadhira kwa jamii inayotokana na huduma za Benki hiyo.
Meneja wa Benki ya Taifa ya Biashara TCB Tawi la Tanga Patrick Swenya ( mwenye suti nyeusi kushoto) akikabidhi msaada wa Vifaa vya Ujenzi kwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga James Kaji ( kulia) Jana kwaajili ya ukarabatI wa Shule Kongwe ya Masiwani, watatu ni aliyeshika Mifuko ya Saruji ni Diwani wa kata ya Majengo Jijini Tanga Salimu Perembo.
"Tulipokea maombi kutoka utawala juu ya kuisaidia shule hii Kongwe na sisi tulilifanyia kazi na leo tumeleta msaada huu ambao utasaidia kufanya ukarabati wa Majengo ya Shule hii" Amesema Swenya.
Ameongeza kuwa Vifaa hivyo vinathamani ya Tsh.Milioni 5,
" Msaada huu unathamani ya Milioni 5 lakini pia tutaendelea kutoa msaada zaidi ya hapa ,Benki yetu ni ya Serikali hivyo tutaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuwaletea Wananchi Maendeleo "Amesema Swenya.
Akipokea msaada huo Mkuu wa ya Wilaya Tanga James Kaji ameishukuru Benki hiyo kwa msaada huo na kuutaka uongozi wa shule hiyo kuutumia vizuri.
"Naomba msaada huu utumike kwenye malengo yaliyopangwa , mdau amejitolea kusaidia ni lazima aone matokeo chanya ya kile alichokitoa , nataka ukarabati uanze Mara moja lakini pia ujenzi wa vyumba vya madarasa ambavyo fedha zake zipo tayari uanze Mara moja " Amesisitiza Kaji.
Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Said Perembo amesema shule hiyo inazaidi ya miaka 80 na majengo yake ni mabovu hivyo wadau wanahitajika zaidi ili kuipata hadhi mpya shule hiyo.
"Hii shule ni Kongwe kuliko Simba na Yanga na imechakaa sana hivyo juhudi nyingi zaidi kutoka Serikalini na Wadau mbalimbali zinahitajika kwaajili ya kuikarabati Shule hii Kongwe na kujenga vyumba vipya vya madarasa" Alisisitiza Perembo.
Amesema kuwa kata yake ina uhaba wa shule ya sekondari nakuiomba serikali kufikiria kujenga.
"Kata yetu haina Sekondari hivyo tunaomba mambo mawili aidha Serikali ifanye mazungumzo na TBA ili watupatie eneo lao ambalo lipo wazi halifanyiwi shughuli zozote au tuibadilishe Shule hii Kongwe iwe Sekondari kwakuwa eneo hili linashule mbili za Msingi katika eneo moja na zote hazina idadi kubwa ya Wanafunzi" Amesisitiza Perembo.
Post a Comment