MBUNGE KOKA ACHANGIA MIFUKO 100 YA SARUJI UJENZI OFISI YA CCM KATA
Na Gustafu Haule, Pwani
MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka (CCM)ametekeleza ahadi yake ya ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Tangini kwa kutoa mifuko 100 ya Saruji huku akisema hajashindwa kujenga ofisi hiyo kama ambavyo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakisema.
Koka, alitoa ahaadi ya kuchangia mifuko ya Saruji 200 katika harambee ya ujenzi wa ofisi hiyo iliyofanyika mapema Julai 02,2023 harambee ambayo ilikuwa ikiendeshwa na mbunge huyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Method Mselewa,akikabidhi mifuko hiyo kwa niaba ya Mbunge huyo ,amesema kuwa mbunge anafanya kazi ya kuwatumikia wananchi pamoja na kuimarisha chama na kwamba suala la kujenga ofisi ya CCM Kata ya Tangini yeye hajashindwa.
Amesema kuwa ,baadhi ya wana CCM wamekuwa wakizungumza maneno ya kumvunja nguvu mbunge juu ya ujenzi huo lakini mbunge yupo imara ndio maana anajitoa kuhakikisha ofisi hiyo inakamilika.
Aidha,Mselewa amewaomba wanaCCM kuendelea kushirikiana na mbunge wao katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika jimbo hilo sambamba na kukijenga chama kwa kukamilisha miradi mbalimbali.
"Mheshimiwa Mbunge aliahidi kuchangia mifuko 200 na leo hii ameleta mifuko 100 kwa ajili ya kuanzia ujenzi na hiyo mingine hata kesho mkisema mnahitaji nayo itakuja maramoja kwakuwa mbunge anapenda kuona chama kinasimama imara,"amesema Mselewa.
Mselewa,amesema mbunge ana majukumu mengi ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo pamoja na shughuli za chama na kwamba haipaswi kumfananisha na mtu ambaye hana majukumu na kwamba yeye anahudumia Kata zote zilizopo ndani ya Jimbo.
"Niwaambie mbunge hajashindwa kujenga ofisi ya CCM Kata ya Tangini,narudia tena kusema, mbunge hajashindwa na hili neno naomba lipigieni mstari vizuri(Bold)maana wapo watu wanaeneza maneno yasiyofaa,"ameongeza Mselewa
Nae Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi CCM Kata ya Tangini Ramadhani Mkwere, akipokea mifuko hiyo amemshukuru mbunge huyo kwa kutekeleza ahadi yake kwakusema CCM Kata ya Tangini bado inaimani kubwa na mbunge huyo.
"Tunamshukuru mbunge wetu Koka kwa kutuletea mifuko hii 100 ya Saruji maana tunaimani kazi ya ujenzi wa ofisi yetu inasongambele lakini tunaomba mbunge hasitochoke kwani ujenzi wa ofisi hii ni endelevu," amesema Mkwere
Hatahivyo, ujenzi wa ofisi hiyo umeanza leo kwa kuchimba msingi kazi ambayo inafanywa na vijana wa hamasa wa CCM Kibaha Mjini pamoja na viongozi wa Chama Kata ya Tangini akiwemo mwenyekiti Anthony Milao na Katibu wake Sophia Mtase.
Post a Comment