HEADER AD

HEADER AD

HOSPITALI ZA HALMASHAURI ZATAKIWA KUWA NA HUDUMA YA UANGALIZI WATOTO WACHANGA


Na WAF - Shinyanga

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amezitaka Hospitali zote za halmashauri nchini kuwa na huduma za uangalizi maalum kwa watoto wachanga (NICU).

Waziri Ummy ametoa agizo ilo Julai 13, 2023 wakati akiongea na timu ya usimamizi wa Afya ya mkoa, wataalam wa Afya ngazi ya jamii pamoja na madaktari bingwa katika hospitali ya Rrufaa mkoa wa Shinyanga.


“Katika mkoa huu wa Shinyanga kuna hospitali za halmashauri sita na vituo vya Afya vya serikali 22, haiwezekani kuwepo na huduma za uangalizi maalum kwa watoto wachanga kwenye Halmashauri Mbili tu, Hapana hili mkalifanyie maboresho haraka”. Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imenunua vifaa vya Tsh. Bil. 6.3 kwa ajili ya huduma za uangalizi maalum kwa watoto wachanga (NICU).

“Sasa ni jukumu letu kuimarisha huduma za watoto wachanga ili mama mjamzito akienda kujifungua basi inapendeza sana atoke na mtoto wake”.

Waziri Ummy ameingeza hata mtoto akizaliwa na gram 500 anapaswa kuishi.



No comments