TIMU YA MCHEZO WA KARATE YA TANZANIA KUSHIRIKI MASHINDANO KONGO
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Mchezo wa Karate itashiriki katika mashindano ya kimataifa ya Nchi za maziwa Makuu nchini Kongo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Julai, Tarehe 17- 23,2023.
Timu ya Tanzania yenye wachezaji 20 kutoka mikoa mbalimbali nchini humo, itashiriki katika mashindano hayo yatakayohisisha nchi zaidi ya 14, Kongo , Angola,nchi za ukanda wa Afrika Mashariki pamoja na nchi Alikwa.
Hii ni Mara pili kwa Tanzania kushiriki mashindano hayo,Mara ya kwanza ni mwaka 2021, ambapo Tanzania Ilikamata nafasi ya pili kwa ushindi wa Jumla, huku Kongo wakiwa wa kwanza.
Tanzania ilipata nafasi hiyo baada ya kuzishinda nchi za Ethiopia, Uganda, Burundi, Somalia, Sudan, South Sudan, Seychelles, Comoros, Mauritius, Djibouti, Eritrea na Rwanda.
Post a Comment