KAMATI YA MAJILIWA YAKUTANA NA WAFANYABIASHARA TANGA
Na Boniface Gideon, Tanga
JUMUIYA ya Wafanyabishara nchini july 26 imekutana na Wafanyabishara wa Mkoa wa Tanga kwaajili ya kusikiliza kero pamoja na kuchukua maoni mbalimbali kwaajili ya kuyapeleka Serikalini.
Hatua hiyo ni agizo la Waziri mkuu Kassimu Majaliwa alilolitoa hivi karibuni alipokutana na Jumuiya ya Wafanyabishara nchini na kuunda kamati maalumu itakayokusanya maoni kila mkoa ili kuweza kuyafanyia kazi ikiwa ni lengo la Serikali kuweka mazingira rafiki katika sekta ya Uchumi.
Akizungumza mara baada ya mkutano huo Mwenyekiti wa jumuiya ya Wafanyabishara nchini Hamis Livembe amesema kuwa pamoja na kuzunguka kila mkoa kwaajili ya kukusanya maoni hayo wana lengo pia la kusajili wanachama wapya katika jumuiya hiyo huku akiipongeza Serikali kuwa kukubali kuwasikiliza wafanyabishara kutokana na kero mbalimbali zinazowakabili na hatimaye kuzipatia ufumbuzi .
“Tumekuwa na ziara za kawaida kuzunguka kila mkoa kwaajili ya kusikiliza kero changamoto na mafanikio yao kutoka kwa wafanyabishara , lakini pia kusajili wanachama wapya na pale wanapokosoa wanakosoa na pale wanapopongeza wanapongeza yale maoni yote huwa tunayachukuwa”.
“Sasa hivi wafanyabishara wana hamu kubwa baada ya lile sakata kubwa la kufungwa maduka kule Kariakoo Dar es salaam, imeundwa kamati baada ya kurudi huko wanataka watusikie kuna nini kipya .
Pia tunatoa mrejesho kwa yale ambayo tayari tumeshapata majibu na viko vingine vichache katika mchakato kwahiyo tunaendelea na ziara ya kuyakusanya maoni ya wafanyabiashara” alisema Livembe
“Tunaweka shukrani zetu kwa serikali kupitia majukwaa yetu ya wafanyabishara kutokana na jinsi walivyotupokea lakini pia walivyofungua milango kwa njia ya mazungumzo na wafanyabishara kwaajili ya kupata muafaka namna walivyotupokea kukaa mezani tujadiliane kwa namna gani bishara zetu ziendeshwe”aliongeza
Kwa upande wake katibu wa Jumuia ya Wafanyabishara wa Mkoa wa Tanga Masoud Ismaili licha ya kuishukuru Serikali amesema kuwa bado zipo changamoto lukuki zinazo wakabiri Wafanyabishara ikiwemo kupandishiwa makadirio ya kodi sambamba na usumbufu wa ushuru kutoka katika taasisi mbalimbali mambo ambayo yanawakatisha tamaa hata ya ulipaji kodi kwa hiari.
“Watu wanalalamika wamepigwa makadirio makubwa ya ulipaji kodi nashauri muwatoze watu fedha kidogo ili walipe kodi kwa wakati na sio kukaa na takwimu ofisini ambazo hazina uhalisia wa Biashara husika.
Ameongeza" ninazo barua za watu mbalimbali wanatozwa kodi kubwa, malalamiko yapo nafikiri wahusika wameyasikia nilikuwa naomba yachukuliwe hatua, Wafanyabishara wote wanataka walipe kodi na sio kukwepa kulipa kodi “ amesema Masoud.
Post a Comment