HEADER AD

HEADER AD

KANDA YA MASHARIKI YAJIPANGA MAONESHO SIKU YA WAKULIMA, PINDA MGENI RASMI



Na Gustafu Haule, Pwani

WAZIRI Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda,anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho ya siku ya wakulima (Nanenane)Kanda ya Mashariki  yanayotarajia kuanza Agosti Mosi Mkoani Morogoro.

Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge, akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa  wanaounda Kanda ya Mashariki ametoa taarifa hiyo Julai 28, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali katika ofisi yake iliyopo mjini Kibaha.







Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge, maonesho ya  Kanda ya  Mashariki yanajumuisha Mikoa mikubwa minne ukiwemo Mkoa wa Dar es Salaam,Pwani ,Tanga na Morogoro.

Amesema kuwa ,maandalizi ya maonesho hayo yamekamilika na kwamba mwaka huu yatakuwa maonesho ya mfano kutokana na kila Mkoa unaoshiriki maonesho hayo kujipanga vizuri pamoja na wadau kuongezeka kwa asilimia 20.

Aidha , Kunenge ameongeza kuwa kauli mbiu ya maonesho hayo ni "Vijana na Wanawake na Msingi Imara na Endelevu kwa Chakula "ambayo inaendana na jitihada za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya uzalishaji na kulisha dunia.

Kunenge,amesema kuwa lengo la maonesho hayo ni kuakisi malengo ya wananchi ili wafikie pale wanapotakiwa na kuongeza tija katika uzalishaji k katika sekta ya kilimo,uvuvi na ufugaji.


"Kanda ya Mashariki mwaka huu tumejipanga vizuri kuhakikisha wananchi wanapata mbinu mpya za uzalishaji katika kilimo,uvuvi na ufugaji na yeyote anayekuja hakika atakuwa ameongeza kwa kujifunza mambo mengi na hivyo kuongeza tija  katika shughuli ,"amesema Kunenge

Amesema kuwa, kila mkoa umekuwa na mkakati kabambe wa kutambulisha mazao mapya ya kimkakati ambapo miongoni mwa mazao hayo ni Muwa,Mkonge,Mchikichi ambapo tayari wameweka mkakati katika kuwainua wakulima kupitia mazao hayo.

Kunenge,amesema kuwa mbali na kuwepo kwa maonesho ya masuala ya kilimo,uvuvi na ufugaji  lakini kutakuwa na wanyama mbalimbali kama vile Simba, Ngamia ,Chui ,Twiga ambapo wananchi wanaweza kufanya utalii maalum .

"Sisi tumeyafanya maonesho yetu kuwa sehemu ya kujifunza mambo mengi,ukiachia masuala ya kilimo lakini pia kutakuwa na utalii mzuri wa wanyama adimu kama Simba na wengineo lakini burudani pia zitakuwepo,", amesema Kunenge

Hata hivyo, Kunenge amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika kutembelea maonesho hayo kwakuwa yapo mambo mengi ya msingi yanayolenga kuboresha Kilimo, ufugaji na uvuvi.

No comments