MADAKTARI BINGWA KUTOKA UJERUMANI KUTUA TANGA
Na Boniface Gideon, TANGA
MADAKTARI Bingwa kutoka nchini Ujerumani wanatarajiwa kuwasili mkoani Tanga Julai 13, 2023 kwa ajili ya kutoa huduma za Kibingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga –Bombo.
Akizungumza na Waandishi wa habari mkoani Tanga jana, Mratibu wa Kambi ya Upasuaji wa Kurekebisha Maumbile (Plastic Surgery) katika Hospitali hiyo Dkt Wallace Karata amesema watakuwepo hadi Julai 28 na siku inayofuatia wataondoka nchini.
Dkt Karata amesema kwamba madaktari hao wanakuja kutoa huduma kwa watanzania ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu lakini pia kwa fani yao ya upasuaji na kurekebisha maumbile ambayo haipatikani vya kutosha nchini itakayotolewa bure kama msaada kwa watanzania.
Amesema hadi sasa wagonjwa 200 wamekwisha kujiandikisha na wakiwa tayari kwa ajili ya kusubiri huduma na Julai 10 ilikuwa ni mwisho kujiandikisha na wageni hao watakapoingia Julai 14 watafanya uchunguzi wa awali na kuweza kupanga ratiba za upasuaji.
Dkt Karata amesema operesheni zitaanza Julai 17 hadi Julai 28 kabla ya wageni hawajaondoka nchini hivyo waliojiandikisha wasishaua tarehe waliozopewa ili kuepukana na usumbufu wa kupanga ratiba zao.
Post a Comment