HEADER AD

HEADER AD

MSHINDI WA KWANZA WA FILAMU KUJINYAKULIA TUZO NA MILIONI 2


Na Andrew Chale, Zanzibar

TUZO ya Nane ya Filamu ya Wakfu wa Emerson Zanzibar (Emerson's Foundation Film Award 2023) inatarajiwa kutolewa usiku wa Julai 2, 2023 katika usiku maalum wa tuzo za filamu za Nchi za Jahazi (ZIFF).

Kwa mujibu wa Mjumbe wa Bodi ya Mfukonwa Emerson Zanzibar,  Salma Adim amesema watatoa tuzo hiyo ambapo mwaka huu inakuwa ni ya nane kwa filamu iliyofanya vizuri zaidi ya zingine.

"Filamu moja tu ndio itaibuka kuwa mshindi ambapo tutamkabidhi tuzo maalum na fedha kiasi cha Tsh 2,000000.(Milioni mbili) na chetu cha ushiriki. 

Lengo kuu ni kuinua vipaji vya wanafilamu wa Kizanzibari kupata kujulikana Kimataifa na kuweza kufikisha kazi zao mbali na ziwe zenye ubora na ufanisi." Amesema Salma Adim.

Wakfu wa Emerson Zanzibar ni shirika ambalo linaongoza katika kuwaenzi watengenezaji filamu mbalimbali na kusaidia vipaji vya wazanzibari kutambulika zaidi na kupata fursa wanazostahiki.

Aidha, tamasha la ZIFF mwaka huu ni la 26 huku likiwa na kaulimbiu ya "Jitambue" ambapo filamu 90 zimeweza kuoneshwa kwa muda wa siku tisa, kuanzia  Juni 24,2023 hadi Julai 1,2023 jana usiku na leo Julai 2,2023.

Jopo la majaji (Jury) wanatarajia kutangaza fimamu zilizoshinda na kuzitunukia tuzo mbalimbali. 


No comments