HEADER AD

HEADER AD

SERIKALI KUENDELEA KUKUZA SANAA NA UTAMADUNI WA TANZANIA

Na Mwandishi Wetu, Chamwino

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dkt.Pindi Chana ameielekeza jamii kupitia makabila yao kuiga mfano wa tamasha la Muziki wa Cigogo katika kuhifadhi, kulinda na kutangaza Utamaduni wa jamii zao.

Balozi Chana amesema hayo wakati wa kufungua tamasha la 14 la Muziki wa Cigogo mapema Julai 22,2023 ambapo amewapongeza kwa hatua ya kuliendeleza tamasha hilo hadi kufika sasa huku likitoa fursa lukuki kwa washiriki. 


"Wizara ninayoiongoza itaendelea kufanya kazi na Chamwino Arts Center (CAC) kwa ukaribu sana katika kuendeleza malengo ya Taifa ya kukuza na kuendeleza Sanaa na Utamaduni wetu.

"Lakini pia nitoe rai kwa waandaaji kuwa wabunifu na kushirikisha wadau wengi wa ndani na nje ili kupata ufadhili uendeshaji wa tamasha hili" amesema Balozi Chana.

Aidha, Balozi Chana amewamwagia sifa wadhamini wakuu wa tamasha hilo wakiwemo Ubalozi wa Uswizi Tanzania na Chamwino Connect USA ambao wamefadhili tamasha.

Katika ufunguzi huo, Balozi Chana ameweza kushuhudia vikundi mbalimbali vya ngoma za kabila hilo la Wagogo ambalo pia limeadhuliwa na watu mbalimbali wakiwemo wananchi wa Kijiji cha Chamwino Ikulu pamoja a viongozi wengine wakiwemo wadau wa Sanaa. 




Awali Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Sanaa Chamwino (CAC) Frank Mgimwa amesema CAC imejiandaa vyema katika kukuza na kuendeleza utamaduni wa Mtanzania kupitia Muziki wa Cigogo wa Kabila la Wagogo ambapo mwaka huu kauli mbiu ni "Kuza Sanaa, Maadili kwanza" amesema Frank Mgimwa. 

Tamasha hilo la siku mbili Julai 22 na 23, linajumlisha Vikundi 40, kati ya hivyo 34 vinatoka mkoa wa Dodoma na mengine 6 yanatoka nje ya Dodoma, vikiwemo kutoka mikoa ya Iringa, Dar es Salaam, Singida na Zanzibar. 
 


No comments