WANAFUNZI SHULE BINAFSI YA RWEIKIZA WALIOFIWA WAZAZI KUENDELEZWA BURE KIMASOMO
>>>Mkurugenzi asema katika shule zao zilizopo Kibaha na Dar es salaam baada ya kutokea mlipuko wa Covid-19, 2019/2020 wazazi 42 walifariki
>>Asema wanafunzi shule ya Rweikiza wataendelezwa bure kimasomo
Na Alodia Babara, Bukoba
MKURUGENZI wa shule ya mchepuo wa kiingereza ya Rweikiza iliyopo Bukoba, Jasson Rweikiza ambaye pia ni mbunge wa Bukoba vijijini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) amesema kuanzia mwaka 2024 na kuendelea wataanza kuwaendeleza bure kimasomo watoto watakaofiwa wazazi wao wakiwa wamesajiliwa shuleni hapo.
Mkurugenzi huyo ameyasema hayo Julai 22, 2023 katika mahafari ya darasa la saba pamoja na awali ambapo amesema mwaka 2021 walianzisha wazo hilo katika shule zao zilizopo Kibaha na Dar es salaam baada ya kutokea mlipuko wa Covid-19, 2019/2020 na kupata changamoto ya kufiwa wazazi 42.
Aliyesimama ni Mbunge (CCM) Bukoba Vijijini Jasson Rweikiza akizungumza na wanafunzi na wazazi katika shule hiyo.
"Wazo la kuwaendeleza kimasomo wanafunzi waliosajiriwa kwenye shule zetu limeshaanza tangu 2021 katika shule zilizopo Kibaha na Dar es salaam baada ya kutokea mlipuko wa Covid-19 2019/2020 na shule zetu kupoteza wazazi 42 na wazo hilo tutaanza kulitekeleza katika shule hii ya Rweikiza kuanzia mwaka kesho 2024" amesema Rweikiza
Mmoja wa wazazi Clara Mirco mkazi wa Muleba amesema mtoto wake Osca Bernadi baba yake alishafariki amemsomesha kwa shida hadi sasa anapofikia wakati wa kuhitimu elimu ya msingi.
Amesema kuwepo wazo la kuwasomesha bure watoto waliofiwa wazazi litasaidia kwani kuna baadhi ya watoto wakifiwa wazazi wanashindwa kuendelea na masomo na kupoteza ndoto zao.
" Wazo la kuwaendeleza kimasomo bure watoto waliofiwa wazazi hapa shuleni litaleta heri kwa watoto kwani kuna wanaoshindwa kuendelea na masomo baada ya kufiwa na wazazi na kupoteza ndoto zao, nikitolea mfano kwangu nilivyomsomesha mwanangu kwa shida baada ya baba yake kufariki" amesema Clara.
Mgeni rasmi katika mahafari hayo ofisa elimu msingi halmashauri ya Bukoba Gregory Fabian amesema wazazi waendelee kuwalea watoto wao kwa maadili mema pamoja na kuwapatia elimu bora ili wapatikane viongozi bora wa badae.
Wa pili kutoka kulia ni afisa elimu msingi halmashauri ya Bukoba ambaye pia alikuwa mgeni rasmi Gregory Fabian akitoa vyeti kwa wahitimu
Kwa mujibu wa risala iliyosomwa na wanafunzi wa darasa la saba shuleni hapo wamesema walianza wakiwa 90 wamehitimu wakiwa wanafunzi 73.
Post a Comment