WAANDAMANA OFISI YA CCM KUILALAMIKIA SERIKALI YA RORYA KUTAKA KUWADHULUMU ARDHI
Na Dinna Maningo, Rorya
NI wananchi wa Kitongoji cha Begi, Kiwandani katika Kijiji cha Majengo, Kata ya Koryo wilaya ya Rorya mkoani Mara, wanaoishi jirani na shamba la mifugo (Utegi Dairy Farm).
Wananchi hao Julai, 27, 2023 majira ya asubuhi waliandamana na kufika ofisi ya Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Rorya kwenda kutoa kero zao dhidi ya Serikali ya wilaya yao kuhusu kutotendewa haki katika zoezi la uthamini wa fidia.
Hata hivyo, hawakufanikiwa kueleza kero zao baada ya kukuta milango ya ofisi ya Chama hicho ikiwa imefungwa kwa kufuli.
Wameiambia DIMA Online kwamba, chanzo cha kuandamana ni baada ya Serikali ya Rorya kutowatendea haki katika zoezi la uthamini wa fidia linaoendelea katika vitongoji hivyo.
Wamewalalamikia wathamini kupima nyumba na mali zilizopo juu ya ardhi huku ardhi ikiachwa bila kuhesabiwa.
Wathamini wadaiwa kuongozana na wanajeshi kwenda kwenye miji yao kufanya uthamini.
Wathamini wadai kufanya uthamini wa mali za wananchi bila kuambatana na Wenyeviti wa Vitongoji
Wathamini wadaiwa kuweka namba kwenye nyumba za wananchi hata kama watu hawapo majumbani huku nyumba zingine zikiachwa kuwekewa namba
Wazee, wajane, waghane, Kaya masikini, yatima,watu wenye ulemavu wa viungo wamwangukia Rais Samia wakimwomba aingilie kati wapate haki zao.
Endelea kufuatilia DIMA ONLINE itakujua mengi yaliyojiri sakata la uthamini wananchi wanaoishi jirani na shamba la Utegi.
Post a Comment