WADAU WAKUTANA KUTATHMINI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA 'TANGA YETU'
Na Boniface Gideon, TANGA
WADAU wa Maendeleo Jiji la Tanga wamekutana kwaajili ya kutathmini utekelezaji wa miradi ya Tanga Yetu ambayo inaendelea kutekelezwa na iliyokwishatekelezwa pamoja na kuweka mikakati ambayo itasaidia kuboresha utekelezaji wa miradi hiyo.
Tanga Yetu imefanikiwa kutekeleza miradi ya maendeleo 17 yenye thamani ya Bil 7 ,baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa bustani kubwa ya pumziko Jijini Tanga maarufu Forodhani yenye thamani ya Bil 1.3.
Ujenzi wa mradi wa ufugaji kuku ambao mpaka mpaka sasa umezalisha kuku 34,000 wenye thamani ya zaidi ya Tsh.Milion 20, ujenzi wa kituo cha Sayansi cha STEM PARK pamoja na Kilimo cha Mwani na ufugaji wa Majongoo Bahari kwa wakazi wa Mwambao wa Bahari.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga James Kaji amewataka wadau wa maendeleo pamoja na wananchi wa Jiji la Tanga kuitunza miradi ya mbalimbali ya maendeleo iliyojengwa na Taasisi ya Tanga Yetu chini ya ufadhili wa Botnar Foundation kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Tanga.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga James Kaji Akizungumza Leo na Wadau mbalimbali wa Maendeleo Wakati wa kikao cha Tathmini utekerezaji wa Miradi ya Tanga Yetu ambayo inaendelea kutekerezwa na ambayo imekwisha malizika.
Akizungumza kwenye kikao cha tathmini utekelezaji wa miradi ya Tanga Yetu kwa wadau wa maendeleo ya Jiji la Tanga,
Kaji amesema miradi hiyo ni mikubwa na kwamba baada ya kumalizika itarudi chini ya usimamizi wa Serikali na wananchi, hivyo ni vyema viongozi na wakazi wa Tanga wakabadilika fikra.
"Tanga bado tumelala na wakati mwingine unajiuliza kwanini linaitwa Jiji ,hebu tuende kwa wenzetu tukajifunze kama Mwanza ,hii miradi ya Tanga Yetu inatakiwa tuitunze sisi wenyewe , wadau wametusaidie sasa sio kila kitu watufanyie ,hebu tuamkeni jamani" amesisitiza Kaji.
Amewataka Madiwani kuwa wakali kwa kuwaadhibu watendaji wazembe "Hapa tumeona baadhi ya watendaji ni wazembe hasa wahandisi kuna miradi mingi ya Halmashauri hasa shule inasua sua.
"Kuna sehemu nimeenda nimekuta mirango ya darasa ukiusukuma unaanguka wenyewe na kuna sehemu nimekuta saruji imeganda haifanyiwi kazi ,sasa nyie Madiwani bado mnaishi nao watendaji wabovu kama hao" amesema Kaji.
Kwa upande wake mwakilishi wa Botnar Foundation Nchini Tanzania ambaye pia ndio msimamizi mkuu wa miradi ya Tanga Yetu Dkt.Hassan Mshindo amesema wamefanikiwa kuwafikia Vijana zaidi ya 100,000.
"Katika kipindi hiki kifupi tumefanikiwa kuwafikia vijana nakuwabadilisha kuanzia kielimu hadi kipato ambapo kwa sasa kila kijana kipato chake kimepanda hadi sh.100,000 kwa wiki.
" Tuna mradi mkubwa wa kuku ambapo hadi sasa umezalisha kuku wengi zaidi ya 30,000 wenye thamani ya Tsh 20,000,000 na fedha zote hizo ni zao Vijana" amesema Dkt.Hassani
Amesema katika miradi ya elimu imewafikia Vijana zaidi ya 2000 ambao walikuwa hawajui kusoma na kuandika lakini pia tumejenga Kituo cha Sayansi cha STEM PARK ambapo Hadi Sasa zaidi ya Vijana na Watoto 34,000 wameshanufaika" amesema Dkt.Hassan.
Post a Comment