MBUNGE RORYA ASEMA WANANCHI HAWAWEZI KUPIMIWA ARDHI, WANAISHI ENEO LENYE HATI
>>Asema watalipwa ardhi kama sehemu ya kifuta jasho na malipo ya ardhi yatakuwa sawa (Flat rate)
>>Asema wananchi wanaishi eneo lenye Hati ya shamba la mifugo ( Utegi Dairy Farm hivyo haiwezekani kupimiwa ardhi.
>>Aeleza makubaliano kikao kilichoketi Julai, 14.
Na Dinna Maningo, Rorya
MBUNGE wa Jimbo la Rorya mkoani Mara, Jafari Chege amesema kuwa Wananchi wa Kitongoji cha Begi na Kitongoji cha Kiwandani, katika Kijiji cha Majengo, Kata ya Koryo hawawezi kupimiwa ardhi kwakuwa wanaishi kwenye ardhi yenye hati ya shamba la mifugo (Utegi Dairy Farm).
Mwandishi wa DIMA Online amezungumza na mbunge huyo kuhusu malalamiko ya wananchi wa Vitongoji hivyo wakiilalamikia Serikali kuendesha zoezi la uthamini wa maendelezo kwenye ardhi huku ikiacha kupima ardhi kwa madai kuwa wananchi walivamia na kuishi kwenye eneo la Serikali la shamba la mifugo (Utegi Dairy Farm).
Pia Mbunge Chege amekanusha kauli ya Wenyeviti wa Vitongoji hivyo na Kijiji kudai kuwa katika kikao kilichoketi Halmashauri ya wilaya ya Rorya baina ya Viongozi ngazi ya Vitongoji, Kijiji, Kata na Serikali ya wilaya hiyo walikubaliana wananchi wafanyiwe uthamini ardhi ipimwe na vitu vilivyo juu ya ardhi kwakuwa siyo wavamizi, kama ilivyoripotiwa DIMA Online, Julai, 29, 2023.
Jafari amekanusha na kusema " kwenye kikao hatukukubaliana kuwa wananchi watapimiwa ardhi, bali walipwe ardhi kama sehemu ya kifuta jasho, na malipo yawe sawa kwa sababu lile eneo tayari lina Hati.
"Kwa hiyo isingekuwa rahisi lilipwe kwa fidia ya ardhi. Mthamini mkuu alitoa ushauri kwamba eneo lenye Hati ni ngumu kulilipa fidia kwa mtu mwingine unalilipaje? yaani ni sawa eneo lako unalimiliki alafu eti Serikali imlipe mtu mwingine anaitwa Juma na wewe unayemiliki ulipwe unaona tofauti hapo?.
Amesema kwakuwa wananchi wameendeleza maeneo hayo wana haki ya kulipwa, watalipwa kifuta jasho cha ardhi na maendelezo baada ya Serikali kuridhia kufanya hivyo.
"Mimi ndiyo niliomba kuwa pamoja na hayo hawa wananchi mnataka kuwalipa uendelezaji tu je wataenda kujenga wapi kama hawalipwi ardhi? kwahiyo Serikali ilikaa chini na baadae ikanijibu kupitia kikao kile.
"Ikanijibu kwamba, basi kama ni hivyo tunafanya uthamini wa uendelezaji alafu tutalipa ardhi kwa wananchi wote malipo sawa (Flat rate) kama ni Tsh. Milioni nne wote watalipwa Tsh.Milioni nne nne, kama ni Tsh. Milioni tano wote hivyohivyo."amesema Jafari.
Ameongeza kusema " Mazungumzo yalishafanyika tayari na Vitongoji vilikuwa zaidi ya vitano, kwingine kote wameshafanya vimekubali, Kitongoji kimoja cha Begi ndiyo kilikuwa na mgogoro.
"Historia zilisemwa, watu wakaleta Documents zao mwishowe tukafika kwenye suluhisho, hatutegemei tena turudi nyuma kwamba nani aliishi, hapa ardhi ya nani, huko tulikuwa tumeshatoka.
"Huko tulishatoka kwakuwa Serikali inahitaji eneo kwa maslahi mapana ya umma na ni kwa mujibu wa sheria" amesema Mbunge Jafari.
>>>Julai, 28, Chombo hiki cha habari kiliripoti habari yenye kichwa cha habarii kisemacho 'WAANDAMANA OFISI YA CCM KUILALAMIKIA SERIKALI YA RORYA KUTAKA KUWADHULUMU ARDHI'.
>>>Julai 30, 2023 iliripoti habari isemayo 'SABABU ZINAZOWAFANYA WANANCHI WASEME SERIKALI YA RORYA INATAKA KUWADHULUMU ARDHI'.
Agasti, 01, 2023 iliripoti habari isemayo 'WENYEVITI WASEMA SERIKALI YA RORYA IMEKIUKA MAKUBALIANO UTHAMINI WA FIDIA' pamoja na habari isemayo 'MADIWANI WASEMA HAKUNA VIKAO VILIVYOWAHI KUJADILI KUWA WANANCHI WA BEGI, KIWANDANI NI WAVAMIZI'.
........... Itaendelea
Post a Comment