MSIMU WA SITA WA ZANZIBAR REGGAE FESTIVAL KUFANYIKA AGOSTI 2024
Na Andrew Chale, Zanzibar
MKURUGENZI wa Tamasha la muziki wa Rege (Reggae) Zanzibar Said Omary Hamad 'Side Rasta' amewashukuru watu wote waliojitokeza kushuhudia tamasha la msimu wa tano.
Tamasha la muziki wa Rege (Reggae) Zanzibar msimu wa tano limefanyika kwa siku mbili Agosti 11 na 13, 2023, Mambo Club ndani ya Ngome Kongwe, Unguja ambalo limefikia tamati usiku wa kuamkia leo huku waandaaji wakitangaza tarehe mpya ya msimu wa Sita kwa mwaka 2024.
"Nawashukuru wasanii wote walipanda jukwaa la Mwaka huu la Zanzibar Reggae Festival. Wadau mbalimbali na wadhamini kwa ujumla shukrani kwa kujitokeza kwenu.
Mwisho wa tamasha hili ni mwanzo wa maandalizi ya tamasha la msimu unaofuata ambao utakuwa ni wa Sita na litafanyika Agosti 9 na 10, 2024 hapa hapa Ngome Kongwe." Amesema Side Rasta.
Aidha, amewaomba wadau kuendelea kujitokeza kudhamini tamasha hilo kuongeza fursa za kiuchumi.
Wasanii mbalimbali wameweza kupanda jukwaa hilo ambapo kwa jana Agosti 12, Wasanii Hussein Masimbi kutoka Bagamoyo Tanzania, Grad Yahaya, Becky Muthoni (Kenya), Kush Riley (Jamaica).
Post a Comment