HEADER AD

HEADER AD

WAZIRI UMMY ATANGAZA NEEMA MATIBABU BURE KUPITIA KAMBI MAALUM


Na Boniface Gideon, TANGA

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga, ametangaza neema ya matibabu kwa baadhi ya magonjwa hususani yasiyoambukiza kwa wakazi wa mkoa wa Tanga na jirani .

Waziri Ummy amewaambia waandishi wa habari, Agasti, 2023, kuwa kwa kushirikiana na Taasisi ya Afya Check na ofisi ya mbunge wa jimbo la Tanga wanatarajia kuzindua kambi maalumu ya kupima Afya bure kwa wakazi wa mkoa wa Tanga na jirani.

    Waziri wa Afya Ummy Mwalimu

Upimaji huo ni kwa siku tano ikiwa ni mpango wa kuitaka na kuihamasisha jamii kuwa na desturi ya kupima Afya mara kwa mara ili pale wanapogundulika kuwa na matatizo mbalimbali waweze kupata matibabu ya haraka.

Amesema kambi hiyo itafanyika kuanzia Augost 21 ambapo wakazi zaidi ya 5000 watafanyiwa uchunguzi huku akiyataja 
magonjwa hayo kuwa ni pamoja na Kisukari, shinikizo la damu, Saratan ya tezi dume kifua kikuu, na magonjwa mengine yasiyoambukiza ikiwemo mlango wa kizazi.

Waziri Ummy amesema kuwa magonjwa yatakayopimwa ni yale yanayoambukiza na yasiyoambukizwa na endapo mtu atakutwa na ugonjwa atapatiwa tiba lakini kwa wale ambao watakuwa na magonjwa yatakayohitaji upasuaji watapatiwa tiba watakapofika madaktari bingwa huku akiipongeza bank ya CRDB ambao ndio wadhamini wakuu wa kambi hiyo. 


Ametaja magonjwa yasiyoambukizwa kuwa ni shinikizo la damu, kisukari, saratani ambapo watapima (mlango wa kizazi, matiti na tezi dume), pamoja na macho lakini pia ameyataja magonjwa ya kuambukizwa kuwa ni virusi vya ukimwi, kifua kikuu na malaria.

"Takwimu inaonesha wapo watu laki mbili ambao hawajajitambua afya zao katika upimaji wa VVU, tunawashauri na kuwahamasisha watu kupima na kama watu wote ambao wana maambukizi wangekuwa wanafuata masharti ya kumeza dawa tunaweza kuutokomeza kabisa" amesema.

"Niwapongeze sana sana wadau wetu wakubwa CRDB, benki yetu kwa kujitolea na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kufadhili huduma zinazowasaidia wananchi" amebainisha.

"Sasa, nitoe wito kwa wananchi wote wa mkoa wa Tanga kujitokeza, wilaya zote kujitokeza kuja kupima katika viwanja vya shule ya sekondari ya Usagara, lengo ni watu 5000 lakini hata tukipata zaidi itakuwa vizuri" amesisitiza.

Mratibu mkuu wa Afya check Isack Maro amesema lengo la kuweka kambi mkoani humo ni kutaka kuwajengea wananchi tabia ya kupima afya kwa hiyari mara kwa mara na hii ni mara baada ya kumaliza mkoani Dar es salaam ambapo zaidi ya wananchi 9324 walifanyiwa vipimo.

"Kitakwimu watanzania tunatumia gharama kubwa sana kujitibu na mara nyingi ni kwa sababu tumechelewa kugundua tatizo sasa kampeni hizi zilianzishwa kuhakikisha kwamba watanzania wanajenga tabia ya kuoenda kupima afya zao mara kwa mara na hii inaonyesha kuyokana na matukio tunayoyaona kutokana na hizi kambi ambazo tumezifanya kwa muda mrefu".

"Kwa sasa hivi ndio tumetoka kumaliza vipimo kwa wakazi wa mkoa wa Dar es salaam na wilaya zake zote na tukafanikiwa kuwapatia huduma za afya za bure wananchi takriban 9324 walifanikiwa kupatiwa huduma zote za kibingwa pamoja na hufuma za kawaida bila kusahau wakapatiwa dawa na vipimo"amesema.

No comments