HEADER AD

HEADER AD

RAIS MWINYI ASEMA SERIKALI YA ZANZIBAR ITAENDELEA KUWAWEZESHA WAKULIMA

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuwawezesha wakulima ikiwa ni pamoja na kutoka fedha kwa ajili ya pembe jeo kwa manufaa ya wakulima.

Rais Mwinyi ameyasema hayo Agasti, 01,2023 wakati akifungua maonesho ya kilimo (Nane Nane) yanayofanyika Kizimbani Dole Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo pia ametembelea mabanda mbalimbali ya Taasisi za Serikali,  binafsi na wajasiriamali, maonesho yatakayohitimishwa Agasti, 10 mwaka huu.

          Rais Mwinyi

Ameongeza kuwa Serikali taendelea kuwakaribisha wawekezaji katika sekta ya kilimo na ufugaji ili iweze kuongeza mchango wake katika pato la Taifa na kuhakikisha usalama wa chakula.

Wakati huo huo, Rais Mwinyi amewahimiza Wazanzibar kuyatumia maonesho hayo ya kilimo kuhimiza Mapinduzi ya kilimo kwa kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa mbinu Bora za kilimo.

Rais Mwinyi amezitaja baadhi ya mbinu bora za kilimo ni pamoja na matumizi ya teknolojia ya umwagiliaji maji, zana za kisiasa kwa madhumuni ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara ili kupata tija zaidi na kuwapa faida kubwa na taifa kwa ujumla.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi amewataka Vijana watumie fursa ya maonesho hayo kujifunza ili wahamasike kujiajiri katika sekta ya kilimo kwani kwa kufanya hivyo watakuwa na uhakika wa uzalishaji wa chakula na kupiga hatua katika maendeleo yao.







     Mke wa Rais Hussein Ali Mwinyi akichuma nyanya 











No comments