TRENI YA KITALII KAMPUNI YA ROVOS YAWASILI TANZANIA IKIWA NA WATALII 31
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imeshiriki mapokezi ya treni ya kitalii ya Kampuni ya ROVOS iliyowasili nchini Tanzania leo ikiwa na watalii 31 wakitokea nchini Angola.
Watalii hao wameonyesha kuvutiwa na mandhali ya maeneo ya Tanzania waliyopita wakati wa ujio wao huo wa Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa na Afisa Utalii Mkuu wa TTB, Alistidia Karaze wakati wa mapokezi ya watalii hao katika kituo cha treni ya TAZARA jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa kundi hilo limejumuisha watalii kutoka nchi za Ujerumani, Uingereza, Marekani na Dernmark.
Afisa Utalii Mkuu, Alistidia Karaze akizungumza na Meneja wa Treni ya ROVOS wakati wa Mapokezi wa treni hiyo jijini Dar es Salaam.Kwa upande wake Meneja wa Treni hiyo, Lyle Ontong amesema safari imechukuwa siku 65 ambapo ilianzia Afrika kusini kuja Tanzania, kwenda nchini Angola na kurudi Tanzania, 2023 kisha kurudi Afrika kusini.
Safari hiyo yenye watalii 67 kutoka Ujerumani ambao wataanzia safari yao katika kituo cha TAZARA jijini Dar nyingine walizopita na kushauri kuwa, watanzania kupaswa kutunza vivutio hivyo vya asili pomoja na mazingira ya miji kwa faida ya vizazi vya baadaye na pia kuwavutia watalii wengi zaidi.
"Treni hii kawaida hufanya safari zake kuanzia nchini Afrika ya Kusini mpaka Tanzania..
Kwa mwaka huu ni safari ya tatu kwa treni hiyo kuleta watalii nchini. Amesema.
Afisa Utalii Mkuu, Alistidia Karaze akizungumza na Meneja wa Treni ya ROVOS wakati wa Mapokezi wa treni hiyo jijini Dar es Salaam.Aidha, Watalii hao 31, wakiwa nchini watatembelea Visiwa vya Zanzibar, Mji wa Kihistoria wa Bagamoyo, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Hifadhi ya Nyerere.
Ujio huo wa Wageni hao ni miongoni mwa matunda ya Filamu ya Tanzania the Royal Tour iliyoasisiwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan inayoendelea kuleta matokeo Chanya na kuvutia watalii kutoka mataifa mbalimbali kuja kutembelea vivutio vya utalii vya nchini.
Watalii wakipiga picha ya ukumbusho mara baada ya kuwasili katika kituo cha TAZARA jijini Dar Es Salaam.
Post a Comment