HEADER AD

HEADER AD

WANAFUNZI WASISITIZWA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI ILI KUPATA UFADHILI

Na Lubango Mleka, Igunga

WANAFUNZI nchini Tanzania wametakiwa kuchangamkia fursa ya kusoma masomo ya sayansi ili kuweza kupata ufadhili katika masomo hayo kwani Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan imeboresha miundombinu ya Elimu hapa nchini inayokwenda sambamba na tekinolojia.

Hayo yamemeelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake CCM (UWT) Taifa na MNEC Zainab Shomari katika ziara yake aliyoifanya Kata ya Bukoko Jimbo la Igunga na kukagua Miradi ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Bukoko na Zahanati ya Ipumbulya.

   Makamu Mwenyekiti UWT Taifa MNEC Zainab Shomari akisalimiana na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Igunga katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo jimbo la Igunga.

Amewataka wanafunzi katika shule hiyo kusoma masomo ya sayansi ili kupata wataalamu mbalimbali watakao kwenda sambamba na sayansi na teknolojia.

"Ninawaomba wanafunzi wote msome kwa bidii kwani nimeambiwa mkoa wa Tabora katika matokeo ya mwaka huu mmefanya vizuri sana, hivyo niwasisitize kusoma masomo ya sayansi ili tupate wataalamu wengi kwani Serikali inatoa fedha nyingi kuboresha Elimu.

"Nimeona mmejengewa maabara nzuri sana ya masomo ya sayansi, jengo zuri la utawala na nyumba za walimu, naomba myatunze majengo haya, pia nitoe wito kwa wazazi kushirikiana na walimu kufuatilia maendeleo ya watoto hawa," amesema Shomari.

Aidha MNEC Shomari amekagua Zahanati ya Ipumbulya ambayo ilipokea kiasi cha shilingi Milioni 50 za ukamilishaji wa boma na miundombinu yake ambapo ameridhishwa na ujenzi huo.



No comments