HEADER AD

HEADER AD

ZUNGU AKABIDHI VYETI KWA WAHITIMU WA PROGRAM YA MAENDELEO YA WASAMBAZAJI YA STANBIC

Na Andrew Chale, Dar es Salaam

NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Hassan Zungu ambaye pia ni Mbunge wa Ilala, ametoa vyeti kwa wahitimu wa  program ya maendeleo ya wasambazaji 'Supplier development program' (Stanbic Biashara Incubator), ambapo wahitimu zaidi ya 100 wamehitimu kozi iliyoandaliwa na Benki ya Stanbic nchini.

Tukio la utoaji wa vyeti limefanyika jana Agosti 26, 2023 Jijini Dar es Salaam ambapo Zangu amewapongeza Stanbic kwa mafunzo hayo huku akitoa neno kwa wahitimu hao kuzingatia elimu walioipata.


"Biashara sio mtaji, Biashara ni taalum ambayo Stanbic benki limeona hilo na kuwapatia mafunzo na taaluma kwenu ili kuwakwamua katika umaskini" amesema Zungu.

Kwa upande wake,  Mkurugenzi wa kitengo cha Maendeleo ya Biashara Stanbic, Fred Max amesema Stanbic Biashara Incubator kusudio sio programu pekee, ni kujitolea kwa hisani na kukuza mafanikio ya miradi ya ujasiriamali. 


"Kupitia safu ya rasilimali na huduma za usaidizi wa biashara, tunalenga kuharakisha ukuaji wa kampuni hizi, tukiwapa zana wanazohitaji ili kustawi.

Ikiwemo ujumuishaji wa mtaji, mafunzo na mwongozo, huduma za kawaida,ufikiaji wa mtandao muhimu wa miunganisho na pia kwa makampuni ya SME ambayo yanachangia maendeleo ya kimkakati ya nchi yetu." Amesema Max.

Ameongeza kuwa:
"Macho yetu yameelekezwa kwenye sekta ambazo zina jukumu muhimu katika ukuaji wa taifa letu kama Kilimo na uzalishaji vifuniko vya ujenzi, kazi za kiraia, na malighafi, Usafiri, Upishi na Hotelier,

"Lakini pia kuuza maudhui ya ndani kwa kuimarisha biashara za ndani, kuwezesha kupata kandarasi na kampuni za kimataifa, kuboresha ufikiaji wa uchumi wa ndani na athari kwa kiwango cha kimataifa pamoja na kushughulikia mahitaji ya msururu wa Ugavi" Amesema.
 


No comments