HEADER AD

HEADER AD

CCM KIBAHA YAPIGA MARUFUKU WAZAZI WANAOWAOZESHA MAPEMA MABINTI

 

Na Gustafu Haule, Pwani

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Kibaha Mjini Mwalimu Mwajuma Nyamka amewapiga marufuku wazazi wenye tabia ya kuwaozesha mapema mabinti zao kuwa waache maramoja kwakuwa watakaobainika hatua kali zitachukuliwa.

Nyamka ametoa kauli hiyo Agosti 31 mwaka huu wakati akizungumza na wazazi,walimu na wanafunzi katika mahafali ya 30 ya Shule ya Msingi Kibaha iliyopo eneo la Tanita Mjini Kibaha.

Nyamka ambaye alimwakilisha mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo,amesema kuwa wazazi wanapaswa kubadilika na wawaache watoto wakike wasome kwakuwa hakuna uridhi mzuri kama elimu.

     Mwalimu Mkuu jina lake ni Martha Kombo maana nimejisahau nikaandika M.Kombo

Amesema kuwa ,wapo baadhi ya wazazi wanatabia ya kuwaozesha mabinti zao mapema kwasababu ya kujipatia mahari jambo ambalo linapelekea kukatisha ndoto za mabinti hao jambo ambalo haliwezi kukubalika.

Aidha,Nyamka amewataka wanafunzi wa kike wasikubali kuolewa kwa matakwa ya wazazi wao bali wapambane na elimu ili wafikie hatua za juu na wakiona mzazi anawashawishi kuolewa ni vyema wakatoa taarifa mapema katika vyombo vya dola ili mzazi husika achukuliwe hatua.

Katika hatua nyingine Nyamka amewataka walimu wasiwapige wanafunzi kwasababu ya kukosa michango ya shuleni kwani jukumu la michango ni la wazazi na sio wanafunzi na kwamba kama wanataka michango ni vyema wakawashirikisha wazazi kupitia mwenyekiti wa kamati ya Shule.

"Wazazi acheni tabia ya kuwaozesha mabinti mapema lakini zingatieni kuwaendeleza watoto wenu kielimu maana urithi pekee ni elimu na hizo mahari hazina tija na CCM imejipanga kudhibiti wazazi wote ambao watagundulika kuwakatisha masomo mabinti kwa kuwaozesha mapema,"amesema Nyamka 

Nyamka,amesema kuwa Rais wa awamu ya Sita Dkt.Samia Suluhu Hassan ameweka kipaumbele katika utekelezaji wa ilani ya CCM na miongoni mwa kipaumbele hicho ni masuala ya elimu ndio maana katika kipindi cha miaka miwili Shule nyingi zimejengwa na zingine zimekarabatiwa.


       Mwenyekiti CCM Kibaha Mjini Mwajuma Nyamka akikata keki katika mahafali ya 30 ya Shule ya Msingi Kibaha .

Amesema,Kibaha utekelezaji wa ilani umefikia asilimia 80 na ilani hiyo ndio mkataba na wananchi ndio maana Serikali inakila sababu ya kutekeleza mkataba wake japo haiwezi kukamilisha mambo yote kwa wakati mmoja lakini kila jambo linafanyika kwa hatua.

"Serikali haiwezi kutatua changamoto zote kwa wakati mmoja ndio maana Kuna "Utatu Mtakatifu" wakiwemo wazazi,Serikali na Shule na kazi ya Serikali ni kujenga Shule, kukarabati Shule na kuwa za kisasa,kuleta walimu na miundombinu mingine lakini hiyo yote ni katika kuboresha elimu", amesema Nyamka

Akijibu risala ya Shule hiyo kwa niaba ya Mbunge Koka Nyamka ,amesema amepokea changamoto ya ukosefu wa dali katika madarasa hayo na kwamba changamoto hiyo itatatuliwa kupitia mfuko wa Jimbo .

Amesema,jambo la madarasa kuwa na dali ni muhimu kwani zitasaidia kupunguza muingiliano wa sauti baina ya darasa moja na lingine na kwamba jambo hilo litafanywa na mbunge kupitia mfuko wake wa Jimbo.

"Mimi nipo hapa kwa niaba ya Mbunge Koka,na amenituma nipokee changamoto zote za shule hii na yupo tayari kutekeleza kwahiyo hata ili la kuweka dali atalishughulikia yeye na kwa kuanza ataanza na darasa la nne na darasa la saba kwakuwa ndio madarasa muhimu ambayo wanamitihani mikubwa mwaka huu"amesema Nyamka

Amesema ,Koka ni mbunge wa wananchi na amekuwa na msaada mkubwa kwa Jimbo la Kibaha Mjini na muda mwingi amekuwa akitumia kutatua changamoto za Jimbo la Kibaha Mjini na kwamba wananchi waendelee kumuunga mkono.


Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo M.Kombo amesema kuwa Shule hiyo ilianzishwa miaka 75 iliyopita lakini mpaka sasa Shule ina wanafunzi 1,425 wakiwemo Wavulana 713 na Wasichana 709 huku wanaohitimu darasa la saba mwaka huu ni 199 wakiwemo Wavulana 99 na Wasichana 100.

Hata hivyo Kombo ameishukuru Serikali ,ofisi ya Mbunge pamoja na diwani kwa kuweza kukarabati majengo ya Shule hiyo yanayoendana tafsiri nzuri ya Mji wa Kibaha huku akiomba juhudi za kusaidia Shule hiyo ziendelee.


No comments