HEADER AD

HEADER AD

RC AYOUB AAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAKULIMA WA MWANI KASKAZINI UNGUJA

Na Andrew Charle, Zanzibar

MKUU wa mkoa wa Kaskazini Unguja, Ayoub Mohammed Mahmoud amewaomba wananchi wa Shehia za Pwanimchangani na Kandwi wanaojihusisha na kilimo cha Mwani kuendelea kuwa na imani na Serikali yao kwani inalifanyia kazi suala lao la mwani kuungua na kukosa soko la uhakika.

RC Ayoub amesema hayo katika mwendelezo wa ziara yake ya Shehia kwa Shehia inayoendelea ndani ya mkoa huo ambapo akiwa Shehia ya Pwanimchangani,  amepokea kero mbalimbali ikiwemo kero kubwa ya wakulima wa zao la mwani ambao wamezilalamikia hoteli kutiririsha maji machafu hali inayopelekea mwani wao kuungua huku pia wakikosa soko la uhakika.


Akijibu kero ya Mwatima Musa Silima wa mkulima wa Mwani la bei za mwani na umwagaji maji machafu kwenye mwani wao, RC Ayoub amesema kuwa umwagaji wa maji unatokana na hoteli kudhibitiwa na watu wa mazingira wa kutomwaga maji baharini.

"Hoteli zinadhibitiwa umwagaji maji mengi baharini, kuna utafiti uliofanyika umetazama haya yote ya maji na bei ya mwani.

"Kwa hiyo tunataraji  kuja na utaratibu mkakati wa namna gani bei ya mwani itaongezeka, Serikali upande wake imeunda kamapuni maalum ya kushughulikia mwani ili upande bei hivyo hili linafanyiwa kazi." Amesema RC Ayoub. 

Pia amesema suala la mwani kutoota vizuri baharini linatokana na suala la mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwa kikwazo cha wakulima kutopata mwani wa kutosha. 


"Tunalo tatizo jingine la mabadiliko ya tabia nchi, limekuwa ni kikwazo kwa wakulima kutokupata mwani wa kutosha.

Mkuu huyo wa mkoa amemwagiza Sheha wa Pwanimchangani kuitisha kikao cha Wananchi kutatua kero zilizopo chini yake ikiwemo ujenzi holela wa hoteli zinazofunga njia pamoja na masuala mengine ikiwemo ukosefu wa ajira kwa vijana katika miradi ya maeneo yao ikiwemo hoteli na shughuli za Kitalii. 



No comments