UWT : TUWALINDE WATOTO DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA
Na Samwel Mwanga, Itilima
IMEELEZWA kuwa ukatili wa kijinsia kwa Watoto umekuwa ni tatizo kubwa hivyo jamii imetakiwa kuwalinda.
Hayo yameelezwa na Mjumbe Wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Taifa,Hawa Ghasia kwa niaba ya Mwenyekiti wa UWT Taifa wakati akihutubia mikutano ya hadhara kwa nyakati tofauti katika Vijiji vya Nkololo,Ngeme na Pijulu katika wilaya ya Itilima mkoa wa Simiyu.
Mjumbe Wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Taifa,Hawa GhasiaAmesema kwamba ukatili wa kijinsia kwa watoto nchini ni tatizo linaloumiza hisia za wengi hasa kwa kuzingatia ongezeko la taarifa kuhusu visa vya namna hii kwenye vyombo vya habari na jamii kwa ujumla ambapo tunasikia ukatili wa kingono wanaofanyiwa watoto wadogo sana kuanzia mwaka mmoja.
Amesema kuwa wapo baadhi ya wanaume wamejitoa ufahamu na kufanya vitendo vya hovyo vya kuwabaka watoto na kuomba watu wote wenyewe tabia hizo wafichuliwe ili hatua za kisheria dhidi yao zichukuliwe.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UWT Taifa,Hawa Ghasia(mwenye miwani)alipitia taarifa ya Maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Msingi Pijuli katika wilaya ya Itilima mkoa wa Simiyu."Dunia imeharibika baadhi ya wanaume wamejizima data na kujitoa ufahamu kwa kufanya vitendo vya ukatili kwa kuwabaka watoto,"
"Vitendo hivyo vya ukatili kwa Watoto vimekuwa vikifanywa na ndugu wa karibu na kuyamaliza kimyakimya jambo hili halikubaliki hivyo ni vizuri tukatoa taarifa kwa vyombo vya sheria ili watu hao washughulikiwe na hao watakuwa tayari wameuvunja undugu,"amesema.
Amesema ni vizuri pia kufuatilia nyendo za Watoto hata wanapokuwa shuleni ili kujua wanafanya nini na hii itatusaidia katika kuwalinda Watoto wetu.
Ameendelea kueleza kuwa kutokana na hulka ya watoto kuwa ni waoga hasa linapokuja suala la kuzungumzia mambo nyeti hasa ya kikatili wanayofanyiwa, hushindwa kueleza moja kwa moja kwa mzazi au mtu yeyote aliyemzidi umri kwa kuhofia kuadhibiwa na yule aliyemfanyia ukatili au huyo anayemfikishia taarifa hiyo.
"Hivyo basi linapokuja suala la kugundua kama mtoto anafanyia vitendo vya kikatili tusitegemee sana Watoto kutueleza Moja kwa Moja kwanza kama Wazazi au Walezi tusipokua wafuatiliaji Wazuri kwenye Maendeleo ya Afya na ukuaji kwa Watoto wetu hasa wenye umri mdogo,"amesema.
Naye Mjumbe wa kamati ya Utekekezaji ya UWT mkoa wa Simiyu,Tinna Chenge amesema kuwa mmomonyoko wa maadili katika jamii umekuwa ni tatizo kubwa kwenye jamii hivyo hatuna budi kushikamana ili tuweze kuwaokoa Watoto wetu ili waweze kufikia ndoto zao za baadaye.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UWT mkoa wa Simiyu, Tinna Chenge akisisitiza jambo katika Mkutano wa hadhara katika Kijiji Cha Pijuli wilaya ya Itilima mkoa wa Simiyu.
Post a Comment