WANANCHI WA FUJONI WAMWELEZA RC AYUB KERO ZINAZOWAKABILI
Na Andrew Charle, Zanzibar
BAADHI ya Wananchi wa Fujoni katika Shehia tatu ikiwemo ya Fujoni, zingwezingwe na kiomba mvua wamefunguka mambo mbalimbali kwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ayoub Mohammed Mahmoud wakati wakiwasilisha kero mbalimbali zinazowakabili.
Awali akitoa kero zake mbele ya Mkuu wa Mkoa, Fatma Haji Machano kutoka Shehia ya Zingwezingwe, amelalamikia kukosa huduma muhimu nyakati za usiku kutokana na kituo cha Afya kukosa nyumba ya Daktari.
"Kumekuwa na kero kubwa hasa wakati wazazi kujifungulia njiani, tunaomba Tujengewe nyumba ya Daktari" amesema Fatma.
Nae Sudi Hamza wa Shehia ya Kiomba mvua ameeleza kero ya miundombinu ya maji, uhalifu wa wizi wa mazao na mifugo jambo ambalo linatishia usalama wao. Pia suala la Bar ya vileo ya Mabatini ambayo imekuwa chanzo cha mmong'onyoko wa maadili.
Kwa upande wake Mariam Mjaka amelalamikia moja ya Bar ya vileo ya mwanamama Mariam ambayo imekuwa ikichangia vitendo viovu ambapo wameomba kuondolewa ili kulinda maadili.
Nae Aziza Mkubwa wa Shehia ya Kiomba mvua, ambaye ni Voluntia wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (Red Cross) amelalamikia ubaguzi wa ajira za muda kwa wao vijana wa huduma ya kwanza katika miradi hiyo a baadala yake wamepewa vijana wengine kutoka mjini.
Kwa upande wake Mbwana Said wa Shehia ya Fujoni, amelalamikia tathimini katika mradi wa maji, ambapo bado hawajalipwa.
"Miradi imepita kwa mashamba yetu, ila hatujalipwa, lakini pia kumejuwa na kero ya kuambiwa kuwa majina yamekosewa katika vyeti vya kuzaliwa watoto huku wakitaka pesa Tsh 20,000 ili kufanya marekebisho, tunaomba suala hili Mkuu wa mkoa uliangalie" amesema Mwananchi huyo.
Nae, Ali Haji Abdalla wa Fujoni amelalamikia ndege aina ya kunguru kuharibu mazao ambapo wameomba namna ya kuona Serikali itadhibiti.
Ali Rashid Ali wa Fujoni amelalamikia hatua ya usafiri wa umma kwa abiria kushushwa nje ya mji hali ambayo inawatesa wanyonge kwa kulipia usafiri zaidi ya mara mbili.
Hata hivyo, RC Ayoub ameweza kupokea maoni na kero hizo za wananchi na kuzitolea ufafanuzi huku kero zingine akiwasimamisha watendaji aliofuatana nao kuzijibu.
Akijibu kero ya uhamiaji, Mrakibu Uhamiaji mkoa wa Kaskazini Unguja Tatu Burhan Mrakibu uhamiaji mkoa wa Kaskazini Unguja amewashauri wananchi kutoa taarifa kwa mgeni yeyote anaeingia katika maeneo hayo.
Amesema licha ya kuzungukwa na bahari bado wananchi wanatakiwa kutoa taarifa kwa viongozi wa maeneo yao juu ya wageni wanaowatulia shaka.
Kwa upande wake, Afisa kilimo Juma Kona Mosi amesema kwa sasa Serikali inaendelea kuchukua hatua katika kilimo ikiwemo kulinda mimea ya zao la mkarafuu ambayo imekuwa ikikumbwa na tatizo la kukauka.
Akijibu kero ya Kunguru amewaomba wananchi kuendelea kutumia njia mbadala kudhibiti tatizo hilo kwani kwa sasa bado Serikali haina mradi mwingine wa udhibiti kunguru kama ilivyokuwa hapo awali.
Post a Comment